

AFISA mkuu mtendaji wa shirika la utendakazi wa serikali ya Donald Trump DODGE, Elon Musk ambaye kwa sasa amenaswa katika kesi ya malezi ya mwanawe mchanga amefichua kiasi anachompa babymama wake.
Musk alishughulikia uvumi huo Jumatatu kupitia X ambapo
alisema kwamba amekuwa akitoa hela za matunzo na malezi ya mwanawe lakini
akadai kwamba hajawahi jua kama mtoto ni wake kweli ama ni anababatizwa.
“Sijui kama mtoto ni
wangu au la, lakini sipingani na kujua. Hakuna amri ya mahakama inahitajika,” alisema.
Bilionea huyo alifichua kwamba babymama kwa jina Ashley alipojifungua,
alimpa $2.5M (Ksh323.13m) na kwamba kila mwaka amekuwa akimtumia hela za
matunzo $500k (Ksh64.63m).
“Licha ya kutojua kwa
uhakika, nimempa Ashley $2.5M na ninamtumia $500k/mwaka.'
St Clair alivunja kimya mara moja, akimwita Musk 'mtoto
mtukutu' ambaye alihitaji kuwajibika.
'Elon, tulikuomba uthibitishe ubaba kupitia DNA kabla hata
mtoto wetu (uliyemtaja) hajazaliwa. Ulikataa,' alisema.
Pia alifafanua kwamba haikuwa kumtumia pesa bali 'kutuma
msaada kwa mtoto wako ambao ulifikiri ni muhimu… hadi ulipoondoa sehemu kubwa
ya hizo ili kudumisha udhibiti na kuniadhibu kwa "kutotii." Lakini kwa
kweli unamwadhibu mwanao tu.'
St. Clair kisha akarejelea hatua yake ya hivi majuzi
mahakamani, jaribio la kumnyamazisha, wakati anachapisha kwenye X.
'Inashangaza kwamba juhudi zako za mwisho mahakamani zilikuwa
kujaribu kunifunga mdomo huku ukitumia chaneli ya mtandao ya kijamii
unayomiliki kihalisi kusambaza jumbe za kashfa kunihusu mimi na mtoto wetu kwa
ulimwengu mzima. Yote ni juu ya udhibiti na wewe, na kila mtu anaweza kuiona.'
Alitoa tusi la mwisho kwa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni
mengi na mshirika wa karibu wa Donald Trump huko Washington: 'Marekani
inakuhitaji ukue, wewe mtoto wa kiume mpotovu.'
Musk bado hajajibu moja kwa moja kwa St. Clair kwenye
mitandao ya kijamii.