
MWANAMKE raia wa Brazil anayedai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanasoka wa Ufaransa Dimitri Payet amewasilisha malalamiko dhidi yake mjini Rio de Janeiro kwa "unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia", kulingana na ripoti ya AFP.
Katika kesi hiyo iliyoangaziwa na France24, mrembo huyo
anayedai kuwa mpenzi wa zamani wa Payet alimnyanyasa kiasi kwamba alilazimika
kunywa mkojo wake mwenyewe ili kudhihirisha mapenzi yake kwake.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 38, ambaye alitumia muda
mwingi wa uchezaji wake na Marseille kila upande wa Ligi Kuu akiwa na West Ham
United, alijiunga na Vasco da Gama mnamo 2023, na kuwasili Rio na mkewe na
watoto.
Kulingana na ripoti ya polisi, ya Machi 29, mwanamke huyo
alisema "alishambuliwa" na Payet, na kumwachia alama kwenye mwili wake,
na kudhulumiwa "kimwili, kimaadili, kisaikolojia na kingono", France24
waliandika.
Mlalamikaji, wakili mwenye umri wa miaka 28 na mfuasi wa
Vasco da Gama, aliiambia AFP kwamba alikutana na Dimitri Payet kupitia
Instagram Agosti mwaka jana, na kwamba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
"Mnamo Desemba, tuligombana kwa mara ya kwanza na
akaanza kuniambia kuwa angeniadhibu," alisema.
"Aliniomba
uthibitisho wa mapenzi, ambao ulikuwa na udhalilishaji. Nilirekodi video
nikinywa mkojo wangu, kunywa maji kutoka kwenye bakuli la choo na kulamba
sakafu," alisema.
Mwanamke huyo pia alidai kuwa wakati mwingine Payet
"alimsukuma" na "kumkanyaga".