Mwanamitandao maarufu wa nchini Brazil amefichua kuwa ndoa yake ilivunjika baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtoto wake wa kambo, ambaye baadaye alimpa mimba.
Rafaela Pedrotti, mwenye umri wa miaka 26, aliambia gazeti la Metropoles kwamba yeye na mtoto huyo wa kambo, ambaye sasa ana miaka 23, walivutiwa kimapenzi walipoanza kuishi pamoja.
"Nilikuwa nimeolewa na baba yake, na tulikuwa tunaishi watatu katika nyumba moja," alisema.
Pedrotti alieleza kuwa uhusiano huo wa kimapenzi uliibuka wakati mumewe alipokuwa akisafiri kikazi na kuacha yeye na kijana huyo nyumbani.
"Mara kwa mara, baba yake alipokuwa kazini na sisi tukibaki nyumbani, kemia fulani ya kimapenzi ilianza kuibuka," alisema.
Pedrotti, anayejulikana pia kwa jina la kisanii DJ Rafaloira, alikumbuka mara ya kwanza kulala na mtoto wake wa kambo baada ya kijana huyo kuanzisha mazungumzo ya kimapenzi.
"Alianza kunitania kwa maneno ya kimapenzi... nami nikaanza kuvutiwa. Mwanzoni nilijizuia, lakini mwishowe tukajikuta tumefanya mapenzi," alisema.
"Tulifanya mapenzi na tukaendelea kwa muda, hadi baba yake alipogundua. Kulikuwa na ugomvi, mzozo, na hapo ndoa yangu na baba yake ikavunjika."
Pedrotti alieleza kuwa yeye na mtoto huyo wa kambo walivutiwa kihisia na walilala pamoja mara ya kwanza walipojaribu.
Mwanamitandao huyo wa miaka 26 alisema kuwa walirekodi maudhui ya watu wazima pamoja na mtoto wake wa kambo na kwamba alibeba mimba. Hata hivyo, alipatwa na mimba hiyo kwa bahati mbaya na baadaye alipoteza mimba hiyo baada ya miezi mitatu.
"Ilikuwa hali ngumu sana. Ni wale tu waliopitia hali kama hiyo wanaweza kuelewa ugumu wake," alisema.
Licha ya hayo, Pedrotti alisema bado ana mawasiliano na kijana huyo na wanapanga kurekodi maudhui zaidi ya watu wazima pamoja.
"Bado tunawasiliana," alisema. "Tutaendelea kurekodi pamoja, lakini baba yake amenikatia mawasiliano kabisa."
Uhusiano huo wa Pedrotti na mtoto wake wa kambo ulizua gumzo miongoni mwa baadhi ya wafuasi wake 371,000 kwenye Instagram baada ya madai hayo kusambaa mtandaoni.
"Je, baba na mtoto wa kambo bado wanaongea?" mmoja wa wafuasi aliuliza.