logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwalimu aliyemuua mume wake aponea hukumu ya kifo

Mwalimu aliyemuua mume wake aponea hukumu ya kifo

image
na

Burudani02 October 2020 - 07:00
Mwalimu mmoja ambaye alimuua mume wake na kuhukumiwa kifo amepunguziwa hukumu hiyo baada ya kukata  rufaa.

Jane Nambuye Manyonge  alihukumuiwa kifo Mei tarehe 30 mwaka wa 2017 na jaji Stella Mutuku baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mume wake  Francis Mulumeti nyumbani kwao  Riruta Dagoretti mwaka wa 2013.

Mulumeti  alikuwa akifanya kazi katika wizara ya ugatuzi ilhali  Manyonge alikuwa mwalimu katika shule ya  Le Pic School mtaani  Dagoretti.

Ikipunguza hukumu yake, mahakama ya rufaa  imesema sio lazima korti itoe adhabu ya juu zaidi ya kifo kama ilivyoratibiwa katika sheria.

Mfano huo mpya  unafaa kutumiwa kwa  kesi baada ya kesi wala haufai kutumiwa kwa kesi zote za mauaji. Wakati  wote wa kesi yake,  mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 51 alikana kumuua mume wake  lakini jaji amesema ushahidi uliowasilishwa kortini  ulimtwika kosa hilo .

Hii ni kwa sababu mshukiwa na mwathiriwa ndio waliokuwa watu pekee katika nyumba yao wakati wa tukio hilo  kabla ya mwanamme huyo kupatikana ameaga dunia. Pia kulikuwa na damu katika nyumba yote na  kuna kisu kilichopatikana na damu katika nyumba yao. Jane pia alitoa taarifa zinazokinzana kuhusu hali iliyopelekea kifo cha mumewe kwani mwanzoni mlinzi wao  wa lango alikuwa amesema kwamba mwanamme huyo alianguka kwenye stuli na kufa lakini baadaye Jane akasema mume wake alikuwa amelalamikia maumivu ya kifua. Baadaye alikiri kwamba walikuwa na ndoa yenye ugomvi .

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved