logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Je Zari Hassan alienda nchini Tanzania kufanya nini?soma uhondo wote

Zari Hassan na wanawe Tiffah na Nillan wamo Tanzania kwa hafla ya kuwasaidia wasichana na sodo.

image
na Radio Jambo

Habari02 June 2021 - 10:38

Muhtasari


  • Zari awasili Tanzania kwa ziara ya kutoa msaada
  • KIla mmoja alitoa hisia tofauti, huku asilimia kubwa na wanamitandao wakisema kwamba ameenda kumuona Diamond
  • Zari Hassan na wanawe Tiffah na Nillan wamo Tanzania kwa hafla ya kuwasaidia wasichana na sodo

Mitandao ya kijamii imeweka motto baada ya wanamitandao kugundua kwamba mwanasosholaiti wa Uganda na mama wa wanawe staa wa bongo Diamond aliwasili nchini Tanzania siku ya JUmanne.

KIla mmoja alitoa hisia tofauti, huku asilimia kubwa na wanamitandao wakisema kwamba ameenda kumuona Diamond.

Haya yanajiri baada ya miezi miwili, baada ya Diamond kuwa Afrika Kusini amabpo alionekana akiwa na wakati mzuri na wanawe.

Pia kuna wale walisema kwamba Zari atarudiana na Diamond na kumuacha mpenzi wake.

Akiwakwenye mahojiano na Wasafi Zari aliweka wazi kwamba wakati staa huyo alipokuwa Afrika Kusini hakuwa analala nyumbani kwake.

Zari Hassan na wanawe Tiffah na Nillan wamo Tanzania kwa hafla ya kuwasaidia wasichana na sodo..

KUlingana na mama huyo wa watoto 5 alisema kwamba atatembelea shule kadhaa na kuwapa msaada wa sodo.

Dakika chache baada ya uwasili walionekana nyumbani kwake Diamond ambapo alisema kwamba siku ya Jumatano ataembelea shule ya Zanaki na timu yake ya Softcare.

Siku chache zilizopita kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Zari aliandika ujumbe huu;

โ€œWakwe zangu wa Tandale mpooo๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹ ilala, Mbagala Temeke Yaan dar nzima bila kuwasahau mashost zangu wa Buza kwa kulengeee alafu namalizia kwa MPALANGE ๐Ÿ‘Œ๐Ÿ‘Œ๐Ÿ‘Œ๐Ÿ‘Œ Nimewamisije sasa๐Ÿ‘ฏ๐Ÿ˜Š๐Ÿ˜Š Team nzima ya SoftCare tunajambo letu, guys are u ready ? Mtoto wa kike kujiamini weee๐Ÿ‘Œ#Softcare sanitary pad! hivi softcare yenyewe inasemaje !!Mimi nasema.... Do le mi go...folevaaaaaa #softcare See you soon Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ ๐Ÿ˜," Aliandika Zari.

Kwa wale sasa ambao walikuwa wanasema kuwa Zari ameenda kumuona Diamond, basi ni wazi kuwa ameanda Tanzania kw ajili ya biashara, na kutoa msaada kwa wasichana.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved