Ngina Kenyatta ajifungua

Ngina alionekana katika hospitali moja hapa jijini Nairobi akiwa ameandamana na mama yake, Margaret Kenyatta.

Muhtasari

• Huyu  ni mjukuu wa tatu wa rais Uhuru Kenyatta na mama wa taifa Margaret Kenyatta.

Ngina Kenyatta bintiye rais Uhuru Kenyatta
Ngina Kenyatta bintiye rais Uhuru Kenyatta

@mpasho

Ngina Kenyatta, ambaye ni binti wa rais Uhuru Kenyatta amejifungua mtoto.

Ngina alionekana katika hospitali moja hapa jijini Nairobi akiwa ameandamana na mama yake, Margaret Kenyatta.

Kulingana na duru katika jarida la Mpasho Ngina alikuwa tayari hospitalini akijifungua.

Ngina hajaonekana katika umma kwa miezi kadhaa na kuibua maswali kuhusu alikokuwa.

Duru pia ziliarifu kuwa Ngina ameolewa kwa mwana wa bwenyenye maarufu nchini Kenya.

Huyu sasa atakuwa mjukuu wa tatu wa rais Uhuru Kenyatta na mama wa taifa Margaret Kenyatta.

Tunamtakia heri njema.