'Rayvanny ni mzuri sana kitandani,' Fayvanny afunguka kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake Rayvanny

Muhtasari

•Fayvanny alisema kwamba hamtamani tena Rayvanny kama mume wake ila kuna baadhi ya mambo ambayo anapeza kuhusu mpenzi huyo wake wa zamani.

•Alikiri kwamba alifurahia sana shughuli yao kitandani wakati walikuwa kwenye mahusiano huku akifichua kwamba Rayvanny alitekeleza jukumu lake kitandani kwa ustadi.

•Alifichua kwamba moyo wake ulivunjika na alilia sana wakati Rayvanny alitambulisha mpenzi wake wa sasa Paula Kajala siku ya Valentines mwaka huu  kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Image: HISANI

Takriban mwaka mmoja baada ya habari kuhusu kutengana kwao kugonga vichwa vya habari, aliyekuwa mpenzi wa staa wa Bongo Rayvanny, Fahyma almaarufu kama Fayvanny amefunguka kuhusu uhusiano wao kabla na baada ya ndoa kuvunjika.

Licha ya kuwa ni dhahiri wawili hao wametangana kikweli, Fayvanny ameweka wazi kwamba angali anampenda sana Rayvanny na kudai kwamba anaamini kuwa mwanamuziki huyo anampenda pia.

Alipokuwa kwenye mahojiano na Wasafi Media, Fahvanny alisema kwamba hana chuki yoyote  dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu huku akieleza kuwa kwa sasa wao ni marafiki wazuri.

"Simchukii nampenda sana. Anajua nampenda, na sidhani kama yeye ananichukia. Ananipenda sana pia. Sisi ni marafiki wazuri" Fahvanny alisema.

Fahvanny alieleza kwamba licha ya kuwa ndoa yao haikufanikiwa wangali wanaunganishwa na  mtoto wao mwenye umri wa miaka minne.

Hata hivyo aliapa kwamba hamtamani tena Rayvanny kama mume wake ila kuna baadhi ya mambo ambayo anapeza kuhusu mpenzi huyo wake wa zamani.

"Ana vitu vizuri sana, mabaya huwa machache. Kuna vitu vingi nakumbuka kumhusu.. kipindi ambacho nilikuwa mjamzito alikuwa ananifanya kama mtoto. Alikuwa ananidekeza sana, alitaka afanye kila kitu yeye. Hakutaka ata niiname ama nishike ufagio. Alipenda kukaanga viazi. Hakutaka nile barabarani" Fayvanny alieleza.

Fahvanny pia alikiri kwamba alifurahia sana shughuli yao kitandani wakati walikuwa kwenye mahusiano huku akifichua kwamba Rayvanny alitekeleza jukumu lake kitandani kwa ustadi.

"Hakuwahi kuwa na tatizo la nguvu za kiume. Yeye ni mzuri kitandani" Alifichua Fayvanny.

Mama huyo wa mtoto mmoja alikiri kwamba moyo wake ulivunjika na alilia sana wakati Rayvanny alitambulisha mpenzi wake wa sasa Paula Kajala siku ya Valentines mwaka huu  kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

"Nilisema asante Mungu, ijapokuwa iliniuma sana lakini nikaona sina sababu ya kuumia. Nilisema asante Mungu  wewe ndio ulimleta na ukamchukua. Nililia sitakuwa muongo. Niliumia sana" Alikiri Fayvanny.

Alisema kwamba kwa sasa hana mahusiano na mwanaume yeyote na kueleza kwamba hako tayari kujitosa kwenye mahusiano mengine.

"Niko single sana. Niko tu kwenye kazi zangu" Alisema