"Tuko salama na wazima" Vera Sidika awatia aibu waliosema angekufia hospitalini pamoja na mtoto wake

Muhtasari

•Baada ya kufanikiwa kujifungua salama kwa njia ya upasuaji mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo sasa amewasuta waliokuwa wanamuombea maovu huku akiwaarifu kwamba yeye pamoja na binitye  wa siku tatu wako hai na salama.

•Vera amesema kwamba mtoto wake ni kila kitu alichowahi kutamani maishani huku akieleza kwamba alitengenezwa kwa mapenzi ya dhati  siku ya wapendanao ya Valentine's.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti mashuhuri nchini Vera Sidika ameendelea kuwatia aibu baadhi ya watu ambao walimtakia maovu alipokuwa mjamzito.

Wiki chache zilizopita mama huyo wa binti mmoja alifichua kwamba kunao baadhi ya watu ambao hawakuridhishwa na ujauzito wake na tangu alipoufichua  walikuwa wanaomba kila uchao msiba umpate.

Vera alisema kwamba kunao watu ambao walisema ujauzito wake ungeharibika punde baada yake kuufichua lakini nguvu za Mola zikamsaidia kuepuka laana zao.

"Wengine hata walisema ujauzito wangu ungeharibika punde baada ya kuufichua. Eti nitapoteza mtoto wangu kama bado hajazaliwa. Mambo mengi. Kama wangekuwa na nguvu nyingi kuliko Mungu , mbona wasiyatekeleze. Sasa tuko na ujauzito wa miezi nane unusu kwa sababu ya Mungu. Kila siku anaendelea kuwatia aibu"  Vera alieleza kupitia ukurasa wake wa Instagram

Siku ya Jumatano wakati Wakenya wengine walikuwa wanaadhimisha siku ya Mashujaa Day mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31 aliweza kujifungua mtoto wa kike aliyepatia jina Asia Brown licha ya  maombi maovu dhidi yake na ujauzito wake.

Alipokuwa anatangaza habari kuhusu kujifungua kwake, Vera alisema kwamba binti yao ataishi kuwa miujuza ambayo itakamilisha maisha yake na mumewe mwanamuziki Brown Mauzo.

"Tarehe 20.10.2021 mida ya saa nne na dakika 21 asubuhi, mtoto wa malkia alizaliwa. Asia Brown @princess_asiabrown. Utaishi kuwa miujiza ambayo itafanya maisha yetu yawe kamili" Vera alisema.

Baada ya kufanikiwa kujifungua salama kwa njia ya upasuaji mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo sasa amewasuta waliokuwa wanamuombea maovu huku akiwaarifu kwamba yeye pamoja na binitye  wa siku tatu wako hai na salama.

Vera amewaambia waliomtakia maovu wapatwe na aibu kuona kwamba maombi yao mabaya hayakutimia kama walivyotaka.

"Kwa wale ambao walisema tutakufia hospitalini wakati wa kujifungua, acha nitumai sasa mnaamini kwamba tunaabudu Mungu aliye hai. Nyote mnafaa mpatwe na aibu popote mlipo. Tuko hai kabisa na Mungu ataendelea kutulinda na kutuzuia na maovu yote. Amina" Vera amesema.

Ameendelea kuwashukuru wote waliomuombea kujifungua salama huku akiwahakikishia kwamba yote yaliendelea vizuri.

"Nashukuru sana kwa maombi yenu. Nilifanikwa kufanyiwa upasuaji salama na nikajifungua Asia. Mimi na mtoto tuko salama na wazima. Tunashukuru Mungu" Alisema Vera.

Vera amesema kwamba mtoto wake ni kila kitu alichowahi kutamani maishani huku akieleza kwamba alitengenezwa kwa mapenzi ya dhati  siku ya wapendanao ya Valentine's.

"Asia Brown, kila kitu ambacho niliwahi kutamani. Mtoto wetu alitengenezwa kwa mapenzi ya dhati siku ya Valentines. Ni mrembo sana. Mtoto mrembo zaidi ambaye nimewahi kuona. Mungu ni muumba kweli" Vera alisema.