"Nimemwaga mayai mengi Ukambani" Mhubiri James Ng'ang'a akiri kuwa na wajukuu kote nchini

Muhtasari

•Ng'ang'a alisema kwamba amepata watoto na wanawake wengi kutoka maeneo tofauti ya Kenya ila mahali alipoonyesha ubabe wake wa kusambaza mbegu ni eneo la Ukambani.

v8FEzbqdLrnganga__1576405445_24852
v8FEzbqdLrnganga__1576405445_24852

Mhubiri mashuhuri James Ng'ang'a  si mgeni kwenye drama za maisha.

Mmiliki huyo wa kanisa la Neno Evangelism Centre amewaacha wengi midomo wazi baada ya kukiri hadharani kwamba ana mamia ya wajukuu ambao wametapakaa kote nchini.

Kwenye video ambayo imeenezwa sana mitandaoni, mhubiri huyo aliyezingirwa na utata mwingi kwenye taaluma yake anasikika akifichulia waumini wake kwamba amezuru maeneo mengi nchini na kuacha kama amesambaza mbegu.

Ng'ang'a alidai kwamba wanaofaa kumuita babu nchini ni wengi kuona kuwa kuna baadhi ya watoto wake ambao tayari ni wazazi pia.

"Niko na watoto wengi. Wengine ni wazee kabisa. Wengine wamejifungua. Mimi ni babu wa watoto wengi sana" Alisema Ng'ang'a.

Ng'ang'a aliweka wazi kuwa amepata watoto na wanawake wengi kutoka maeneo tofauti ya Kenya ila mahali alipoonyesha ubabe wake wa kusambaza mbegu ni eneo la Ukambani.

Alikiri kwamba huwa anakumbana na watoto wengi ambao huwa anawashuku kuwa wa damu yake kila anapozuru eneo la Ukambani.

"Wengine wako Kirinyaga, wengine wako Ukambani, wengine wako Mombasa, wengine Nakuru. Kisumu sina namba nzuri sana, sikuwa nimepata huko Kisumu, labda mmoja mmoja yule alikaa Mombasa. Lakini Ukambani nimemwaga mayai. Ukambani nilitega mayai kabisa. Ata huwa naenda Ukambani naona hii ni kama yangu" Ng'ang'a alisema.

Wiki kadhaa zilizopita mhubiri huyo alikiri kuwa na watoto zaidi ya 70 kote nchini.

"Mimi huwa naambia watu niko na watoto kama sabini hivi. Ukambani kama 30, Ukienda Mombasa kama ishirini na kitu hivi, huko Murang'a  na Nyandarua" Ng'anga alidai

Ng'ang'a alisema kwamba alifanya majaribio mengi ya ndoa ila hakuwa anapata mafanikio kwani kila alipojaribu alikuwa anajipata akitengana nao baada ya muda ama kitu kingine kutokea na kufanya uhusiano ufikie kikomo.

"Mwingine alienda akiwa na ujauzito wa miezi sita. Alisema ameenda kuchua nguo lakini hakurudi" Alisema.