Rais Suluhu awataka wanaume kuwaripoti wanawake ambao wanawaomba pesa

Muhtasari
  • Asilimia kubwa ya wanaume wamepongeza usemi wake Suluhu, kwani wamepunguziwa mzigo

Siku ya Alhamisi rais wa Tanzania Samia Suluhu alivutia wanaume wengi  baada ya kuwahimiza  kutoa ripoti ya wanawake ambao huwauliza au kuwaitish pesa kabla ya kufunga ndoa.

"Wanaume, kama wanawake ambao sio wake wakowanakuitisha pesa ripoti kwenye kituo cha polisi," Suluhu alisema.

Taarifa  hiyo kutoka  kwa Suluhu imekaribishwa na wanaume kwenyemitandao ya kijamii ambao wamekuwa waathirika wa 'kutuma nauli' na 'kulipa kodi'.

Asilimia kubwa ya wanaume wamepongeza usemi wake Suluhu, kwani wamepunguziwa mzigo.

Awali Samia aligonga vichwa vya habari, baada ya kuwakejeli wanawake ambao hawana matiti.

Baada ya usemi wake alipokea kejeli nyingi kutoka kwa wanamitandao hasa wanawake, huku baadhi yao wakiddai kwamba usemi wake uliwaghadhabisha.

Ni tabia na mazoea ya baadhi ya wanawake kuitisha wanaume pesa na kisha wanawaaacha wakiwa wamevunjika moyo baada ya kupata walichokuwa wanataka.

Wanaume wengi wamekuwa waathiriwa wa kutuma nauli, na kughaiwa na wanawake na pesa zao huku wakisalia mikono mitupu.

Je rais Samia aliwaokoa wanaume, kama wanavyodai?