"Najihisi mjinga na ninaumia moyoni!" Monica Ayen amtema Eric Omondi baada ya wiki mbili tu

Muhtasari

•Ayen amesema kwamba alisikitishwa na kuvunjwa moyo sana na ujauzito bandia ambao Omondi alidai kapachika Miss P pamoja na mvurutano wake na Jackie Maribe uliohusisha mtoto.

•Mwanamitindo huyo amemshtumu Omondi kwa kuchukua fursa ya uvumilivu wake huku akilalamikia uongo wake mwingi usioisha. 

Eric Omondi na Monica Ayen
Eric Omondi na Monica Ayen
Image: INSTAGRAM

Mshindi wa Wife Material Monica Omondi ameghadhabishwa na matendo ya mchekeshaji Eric Omondi ambayo yameibua gumzo kubwa hivi karibuni. 

Mwanamitindo huyo kutoa Sudan Kusini ametumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza ameamua kukatiza uhusiano wake na Omondi kufuatia drama zilizomuandama kwa kipindi cha takriban wiki moja kilichopita.

Ayen amesema kwamba alisikitishwa na kuvunjwa moyo sana na ujauzito bandia ambao Omondi alidai kapachika Miss P pamoja na mvurutano wake na Jackie Maribe uliohusisha mtoto.

"Ilikuwa ule ujauzito bandia kwanza nikaelewa, ikaja drama zako na baby mama na sasa hauko nyumbani. Hii yote ni nini??  Mimi sio msichana yule wa kuketi tu na kusubiri upoteze wakati wangu. Nitaenda hivi karibuni . Shukran kwa kujaribu kunitunza lakini. @ericomondi tunza Wife Material wako mwingine vizuri ama hutawahi tulia!!" Ayen aliandika.

Mwanamitindo huyo amemshtumu Omondi kwa kuchukua fursa ya uvumilivu wake huku akilalamikia uongo wake mwingi usioisha. 

Ameapa kwamba hakuna chochote kitakachoweza kutuliza moyo wake unaoumia kwa sasa huku akidai hayakuwa mapenzi yake kujipata katika hali ile.

"Nimesikitika tena tena kwa kuwa kweli alijua nilikuwa mvumilivu akajinufaisha. Ni kweli kwamba nilimuunga mkono hata kama alikosea. Alinileta kutoka kwa nchi yangu kuja kunifanya nijisikie kuwa lazima nipigane ndio nipate njia ya kuingia moyo wake. Najisikia mjinga na naumia moyoni hivi sasa nikiwa nimewekwa  katika hali hii ambayo sikuwahi kuuliza. Hata kama uliishi kusema nakupenda nakupenda, haitarekebisha chochote au kurudisha chochote nilichopoteza. Nachukia ukweli kwamba ulinidanganya na ndio maana sitaki ndoa hii au uhusiano wowote kati yetu uendelee kwa sababu nilikuambia tangu mwanzo kwamba siwavumilii waongo!!" Ayen aliandika.

Haya yanajiri wiki mbili tu baada ya Eric Omondi kumtangaza Ayen kuwa mshindi wa shoo yake ya mwisho ya Wife Material huku akidai kwamba yeye ndiye aliyenasa moyo wake kwani alitimiza yote aliyokuwa anatafuta kwa mke.

Omondi aliapa kufunga ndoa na mwanamitindo huyo kutoka Juba na kuishi maisha yake yote pamoja na yeye kwenye dhiki na faraja

"Monica Ayen-Omondi. Hongera kwa kushinda moyo wangu. Hongera kwa kushinda shoo ya mwisho ya Wife Material. Naahidi kukupatia mapenzi yangu yote. Nitakuheshimu. Nitakuheshimu kwa utu wangu wote. Naahidi kukulinda. Siwezi kusubiri kuanzisha familia pamoja nawe. Siwezi subiri kupata watoto warembo na wewe. Wewe sio tu mwanamitindo bali una moyo mzuri. Unanikamilisha kipenzi. Unanikamilisha mpenzi wangu" Eric alitangaza.

Mchekeshaji huyo alishukuru taifa la South Sudan kwa kumpa malkia wa ufalme wake huku akiahidi kumlinda na kumpatia mapenzi yasiyoisha