"Ya kale hayanuki, angazieni muziki!" Ringtone Apoko atoa ushauri kwa Diana Marua, Willy Paul na Bahati

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo ambaye sio mgeni katika sarakasi mitandaoni alishauri Diana, Bahati na Willy Paul kutoangazia yaliyotendeka kitambo.

•Ringtone pia aliwashtumu Bahati na Willy Paul kwa kupata watoto wengi na wanawake mbalimbali hapa nchini.

Willy Paul, Diana Marua na Bahati
Willy Paul, Diana Marua na Bahati
Image: INSTAGRAM

Mwenyekiti wa muungano wa wanamuziki wa nyimbo za injili wa kujibandika Alex Apoko almaarufu kama Ringtone ametoa kauli yake kuhusiana na  drama ambazo zimekuwa zikienea mitandaoni baina ya  Diana Marua, Willy Paul na Bahati.

Akiwa kwenye mahojiano na Nicholas Kioko, Ringtone aliweka wazi kwamba hajui chochote kuhusu madai ya unyanyasaji wa kingono yaliyotolewa  na Diana Marua dhidi ya Willy Paul.

Ringtone hata hivyo alisema yale ambayo tumekuwa tukisikia kati ya Willy Paul, Diana na Bahati si ya kushangaza kwa kuwa wanajihusisha na usanii wa kidunia wala sio injili.

"Mimi sijui chochote kuhusu mambo ya kunajisiana. Sijaelewa kwa sababu mimi naangazia mambo ya ufalme wa Mbinguni ila ninachojua ni kwamba ukienda kwa mambo ya shetani vitu ambavyo vitatoka si vya kupendeza. Injili inamaanisha habari njema. Mambo ya Mungu ni habari njema, mambo ya dunia ni habari mbaya. Diana, Bahati, Willy Paul ni watu wanatumikia Shetani. Tunasikitika sana wasanii wa shetani wanatuaibisha" Ringtone alisema.

Mwanamuziki huyo ambaye sio mgeni katika sarakasi mitandaoni alishauri Diana, Bahati na Willy Paul kutoangazia yaliyotendeka kitambo.

Aliwashauri watatu hao waangazie mambo mengine yanayofaa badala ya kuangazia madai kuhusu mambo yaliyotendeka zamani.

Ringtone pia aliwashtumu Bahati na Willy Paul kwa kupata watoto wengi na wanawake mbalimbali hapa nchini.

"Ningemshauri Diana B kama mtu mzima nimwambie  kama ni kitu ilitendeka kitambo amuombee Willy Paul na umwachie Mungu. Mwili tulipewa na Mungu, si wetu. Ingekuwa ni kitu ya sasa hivi tungekuwa tunaongea mambo tofauti. Kama ni kitu ya kitambo, nataka hao wasanii watatu waangazie vitu vuinavyofaa kwa kuwa wana jukumu la kuwatumikia Wakenya. Diana ako na watoto wadogo, Willy ako na watoto wadogo. Ako na watoto kama ishirini huko nje, pia Bahati ana watoto kama ishirini. Wa Diana ni wachache na kuna wengine amezaa na wanawake wengine. Hao wanaume ukiwaweka pamoja wako n watoto kama hamsini. Kila mmoja wao amezalisha wanawake wengi sana. Hayo  mambo wanatuletea sasa havi waache. Kama ni mambo yanatendeka sasa hivi yasemwe, lakini kama ni kitu ya kitambo tusahau tujenge taifa... Diana B ningependa kukashauri uangazie mambo chanya. Mavi ya kale hayanuki! Willy Paul pia nawe tunajua ni msherati, wacha kutwambia vitu ambavyo havitusaidii, Bahati pia wacha kujaribu kutufanya tukuhurumie. Tunajua uko  na wanawake wengi. Hii mambo yote tukiweka pamoja hakuna mtu asiye na hatia. Angazieni muziki Willy Paul achana na Diana. Ata kama ulimkula alichukuliwa na mwenye anamkula kila siku. Kwani ni wivu? Angazieni mambo yenu ya shetani mtuachie Mungu!" Ringtone aliwashauri.

Wiki iliyopita Diana Marua alijitokeza mitandaoni kumshtumu Willy Paul kwa kujaribu kumbaka, madai ambayo Paul alipuuzilia mbali.