logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Miss P asema anatamani kukutana na Otile Brown

Katika mahojiano na kipindi kimoja cha habari   ameeleza  kwamba mwanamuziki anayependa kusikiza kazi zake na angetamani sana kukutana naye angalau wazungumze ni Otile

image
na

Yanayojiri03 February 2022 - 05:22

Muhtasari


•Miss P  amefunguka na kueleza nia yake ya  kutaka kukutana na msanii sifika humu nchini Otile Brown

•Katika mahojiano na kipindi kimoja cha habari   ameeleza  kwamba mwanamuziki anayependa kusikiza kazi zake na angetamani sana kukutana naye angalau wazungumze ni Otile

Miss P

Msanii  wa kike  Miss Picasah almaarufu Miss P  ameelezea nia yake ya  kutaka kukutana na msanii sifika humu nchini Otile Brown.

Katika mahojiano na kipindi kimoja  alisema kwamba anapenda kusikiza kazi zake Otile na angetamani sana kukutana naye angalau wazungumze.

"Natamani nikutane na Otile Brown kwa sababu naona tunawiana kitabia, ananipa hamu ya kutamani sana kumuoana," alisema Miss p.

Miss P  ni msanii chipukizi ambaye alijulikana wakati alitangaza kuondoka kwa lebo ya Saldido ya Willy Paul.

Baadhi ya nyimbo za Miss P ni; Baby shower, single, Liar na Mashallah.

Aidha alisisitiza kwamba kamwe hawezi kurudi kufanya kazi yoyote na msanii Willy Paul, ikifahamika kwamba Miss P alikuwa chini ya Saldido Record ila baadaye wakatengana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved