logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aunty Ezekiel na Jacqueline Wolper wasutwa kutoka kimapenzi na vijana wadogo

Maoni: Kwa tamaduni za Kiafrika huu utaratibu haupo kabisa, umeletwa na Na watu wachache wanaoiga kila ujinga wa nchi za Magharibi

image
na Radio Jambo

Habari22 April 2022 - 06:09

Muhtasari


• Hulka ya kina mama kutoka na vijana wadogo kimapenzi imetajwa kuwa uraibu wa kutizama ponografia za wazungu.

Aunty Ezekiel, Jacqueline Wolper na wachumba wao wachanga

Waigizaji wakongwe wa Bongo Movie Jacqueline Wolper na Aunty Ezekiel wamejipata katika jungu la moto wa tanuru kwa kudanga au kutoka kimapenzi na wanaume wadogo kiumri kuwaliko.

Ameandika jamaa mmoja kwa jina Hopeman David kupitia Instagram yake kwamba wawili hao katu hawana hata chembe ya aibu kutembea na vijana wadogo. Jambo hilo linawaondolea heshima kubwa waliyohangaika kuipalilia enzi wakiigiza na nguli wa uigizaji marehemu Steven Kanumba.

“Haya ni maajabu ya Dunia, Dunia inaelekea Kufika Mwisho, hivi inakuaje Mwanamke, mzima kabisa wa akili, anatoka kimapenzi na vijana wadogo? Hivi Sura huwa wanazificha wapi wakati wa kwichi kwichi? Maana ni aibu kubwa hizi,” alilalama mdau David.

Pia hakuwasaza vijana hao wadogo wanaokubali kutumika kimapenzi na kina mama hawa waliokolea kiumri na kusema kwamba pengine vijana hao wanaiona kama fursa ya kushusha kitonga ilimradi maisha yasonge kutokana na umaskini uliokithiri.

Lakini pia aliwakashfu na kujiuliza maswali mengi kwamba hata vijana hao kwani hawaoni aibu kutangamana na utupu wa wanawake wakubwa kiumri wengine rika za wazazi wao bila soni.

Sababu nyingine ambayo imekisiwa kwa hulka hii ya vijana kutoka kimapenzi na kina bibi ni madhara ya kudanganywa na wazungu kupitia picha zao za utupu almaarufu ponografia.

“Pia Vijana wa kiume huwa wanatoa wapi ujasiri wa kukaa utupu mbele ya mwanamke mtu mzima? Haya yote ni madhara ya kuangalia sana Ponografia. Kwa tamaduni za Kiafrika huu utaratibu haupo kabisa, umeletwa na Na watu wachache wanaoiga kila ujinga wa nchi za Magharibi. Endeleni kudanganywa na wazungu kwamba mapenzi sio Umri, umri ni namba tu,” David aliandika.

Ila pia alionekana kuegemea kidogo kwa mtamazo wake kwamba ni vizuri kina babu kutoka kimapenzi na mabinti wabichi kama jani la mgomba kuliko vijana wadogo kutoka kimapenzi na ajuza.

Maoni yako ni yepi?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved