logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Najililia mwenyewe-Aliyekuwa mpenzi wake Stivo Simple Boy akiri kupambana na msongo wa mawazo

Pritty alionekana kufanya vyema kulingana na picha zake za Instagram

image
na Radio Jambo

Burudani09 May 2022 - 11:00

Muhtasari


  • Aliyekuwa mpenzi wake Stivo Simple Boy akiri kupambana na msongo wa mawazo

Aliyekuwa mpenzi wa Stivo Simple Boy , Pritty Vishy ametumia ukurasa wake wa Instagram kukiri kwamba anapambana na msongo wa mawazo.

Anasema kuwa kupambana na unyogovu ndio jambo gumu zaidi kufanya kwani watu wanaweza kufikiria kuwa uko sawa kwa sababu unatabasamu nao lakini unalia peke yako.

Pritty Vishy na mwimbaji Stivo walikomesha uhusiano wao ambao sio wa muda mrefu sana miezi michache iliyopita.

Pritty alionekana kufanya vyema kulingana na picha zake za Instagram na hata alifanikiwa kupata kazi ya ubalozi.

"Kujaribu kupambana na unyogovu 😪ndilo jambo gumu zaidi hili... inabidi uonekane sawa wakati hauko sawa..lazima utabasamu ukiwa nao..kitu pekee ninachofikiria kufanya vizuri zaidi ni kulia peke yangu na kulia. tabasamu nao kama ila kitu kiko sawa lakini hakiko sawa😔😔😔," Pritty Amekiri.

Mashabiki walitumia fursa hiyo kumfariji Pritty.

Awali akiwa kwenye mahojiano, mwanadaa huyo alisema na kukiri kwamb akiwa kwenye uhusiano na msanii huyo alimcheza na wanaume wengine.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved