logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ex wangu alikuwa na wanaume zaidi ya 50,'Stivo Simple Boy afichua

Zaidi ya hayo, amezua taharuki mtandaoni alipomuuliza kuhusu uhusiano wake wa sasa na Prity Vishy.

image
na Radio Jambo

Burudani06 June 2022 - 12:00

Muhtasari


  • Simple Boy alisema kuwa Pritty Vishy ni aina ya msichana ambaye anapenda sana mwanaume anayekuja karibu naye na ameshindwa kujiheshimu kwanza
Pritty Vishy, Stivo Simple Boy

Mwanamuziki Stivo Simple Boy hahitaji kutambulishwa, hii ni kwa sababu amekuwa akivuma hivi karibuni.

Akiwa kwenye mahojiano siku ya Jumatatu  Stivo Simple Boy alieleza upande wake wa hadithi na yale ambayo amekuwa akipitia hivi majuzi.

Zaidi ya hayo, amezua taharuki mtandaoni alipomuuliza kuhusu uhusiano wake wa sasa na Prity Vishy.

Simple Boy alisema kuwa Pritty Vishy ni aina ya msichana ambaye anapenda sana mwanaume anayekuja karibu naye na ameshindwa kujiheshimu kwanza.

Alisema mpenzi wake huyo wa zamani amelala na wanaume 50 ambao anawafahamu na baadhi yao ni marafiki zake.

Pia alimshutumu mpenzi wake wa zamani Prity Vishy kwa kusema kuwa sababu kwa nini hataki warudiane ni kwamba yeye ni aina ya mwanamke ambaye haelewi mtu hata kidogo.

Aidha msanii huyo alidai kwamba walipatana na Pritty alipokuwa kwenye shule ya msingi na kumshauri asome kwani atamsubiri,ilhali Pritty hakufanya hayo.

Huku akizungumzia usimamizi wake wa muziki wa awali, msanii huyo alikana madai kwamba ulikuwa unamnyanyasa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved