logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nandy afunguka sababu za kukana ujauzito wake

Alisema walipanga kutangaza ujauzito pamoja na mradi wake mwingine.

image
na Radio Jambo

Michezo11 July 2022 - 10:07

Muhtasari


•Nandy amesema kuwa alifikia hatua ya kuuanika ujauzito wake kwa sababu alichoka kuukana kila alipokuwa akihojiwa.


Msanii wa bongo fleva Nandy akiwa na mume wake mtarajiwa Nenga

Nandy ambaye ni msanii mkubwa wa kike nchini Tanzania anasema kuwa alifikia hatua ya kuuanika ujauzito wake kwa sababu alichoka kuukana kila alipokuwa akihojiwa.

''Wakati nafanya mahojiano na kumkana mtoto wangu, nilikuwa nikijisikia vibaya huku nikidanganya kuwa sina mimba.”Nandy alisema katika mahojiano na Bona TV.

Nandy au Mama Nenga alisema kuwa; “Nadhani tulitaka kuweka wazi ujauzito pamoja na projekti yangu nyingine. Lakini pamoja na mambo yote hayo, bado nimebaki kuwa msanii na maisha lazima yaendelee. Siwezi kuendelea kuficha ujauzito kila wakati''

Akihojiwa na Bona Tv, mwanamuziki huyo alibainisha kuwa mimba ni kitu ambacho hakifichiki.

Aidha alibainisha kuwa kando na usanii yeye ni mumewe pia ni wafanyibiashara.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa ,miradi mingi walikuwa wakipata ya kufanya kazi au biashara na Makampuni zingine na  hangeweza kuficha mimba yake  tena kwani ilishakuwa kubwa

“Ujauzito ni baraka na unavyojua kuna watu wengi wanahangaika kutarajia kuwa wazazi, tunawaombea wote, kwasabau ya  kazi zetu sikuweza kujificha tena kwani kazi bado ilikuwa inanihitaji''  alisema.

Katika mahojiano hayo Nandy alisema kuwa hakuna kitu kizuri kama kupata mtoto mtu akiwa ndani ya ndoa. Alisema hata hivyo alijawa na furaha licha ya kupata ujauzito ka hajaingia kwa ndoa rasmi.

''Mpango yetu ya harusi ilikuwa imepangwa kabla atakujua kuwa nina ujauzito,tukaendelea na ratiba zetu za kawaida kwasababu haitufungi, mimi nilitamani nipate mtoto, nikiwa ndani ya ndoa, lakini Mungu kanijalia mimba kabla ya ndoa yenyewe,huu mtoto nitaingia naye kwenye harusi  na nitaingia naye ndani ya ndoa'' Nandy alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved