Sandra Dacha: Mimi na Akuku Danger hatuwachani, tuko locked

Sandra Dacha amekuwa akimshughulikia Akuku Danger kwa ukaribu mno haswa kipindi analazwa hospitalini.

Muhtasari

“Sijasema kwamba mimi ni mpango wa kando, ilikuwa tu msemo, nukuu tu" - Sandra Dacha

mchekeshaji Akuku Danger na mpenzi wake muigizaji Sandra Dacha
mchekeshaji Akuku Danger na mpenzi wake muigizaji Sandra Dacha
Image: Akuku Danger (Facebook)

Muigizaji bonge, Sandra Dacha sasa amesafisha mawimbi na kuwaacha wambea wakikimbilia mafichoni baada ya kuweka wazi kwamba yeye na mchekeshaji Akuku Danger katu hawawezi wachana ije mvua, lije jua bado wao ni wapenzi mpaka siku ya Kiyama.

Katika maohiajo ya kipekee na kituo kimoja cha redio nchini, Dacha alisema kwamba ni pole kubwa kwa wale wote waliokuwa wanafikiria kwamba wataachana, haswa baada ya vita vya mitandaoni kutupiana maneno fiche baina yake na Akuku Danger.

Dacha alisema kwamba ule ujumbe alioachia kwenye Facebook yake akimtaka Akuku Danger aache kupakia picha za mkewe kila mara ulitafsiriwa vibaya na watu aliowaita wambea.

“Akuku Danger hatuwezi wachana, bado tuko locked. Ule ujumbe mimi nilisema tu, Wakenya mna umbea mwingi sana, pale mimi nilisema tu, hiyo nimemwambia nini,” alisema Sandra Dacha.

Pia alionekana kuuasi ujumbe wake katika kila neno ambapo alikanusha kwamba yeye si mpango wa kando kama ambavyo aliandika kwenye ujumbe ule wake.

Dacha alisisitiza kwamab ujumbe wake ulieleweka visivyo na kusema kwamab kwa kutaja maneno ‘mpango wa kando’ haina maana kwamba yeye ni mpango wa kando bali alitumia tu kama msemo.

“Sijasema kwamba mimi ni mpango wa kando, ilikuwa tu msemo, nukuu tu. Mimi na Akuku ni wapenzi na nyinyi mtabakia kuwa watazamaji,” alisisitiza sana Sandra Dacha.

Muigizaji huyo mwenye umbile la kibonge pia alizungumzia hali ya afya ya Akuku Danger ambapo alisema kwa sasa yuko sawa kiafya na kusema wanaomba sana asirudi tena hospitalini kwa sababu tangu Desemba mpaka sasa Julai mchekeshaji huyo hajapata kufanya kazi kutokana na afya yake kudorora.

Aliwashukuru Wakenya sana kwa kusimama na Akuku Danger kumtolea mchango wa kulipa ada ya hospitalini kwa mara mbili ambayo mchekeshaji huyo amelazwa.

Juzi Muigizaji huyo alipakia picha ya mwanawe wa miaka 8 akimsherehekea siku yake ya kuzaliwa , jambo lililowashangaza wengi ambao hawakuwa wanajua kama ana mtoto. Kweney mahojiano hayo, alisema mwanawe anaitwa Jiwel Israel na kufichua kwamab alikuwa anasherehekea miaka 8 tangu kuzaliwa kwake.