Fahamu baadhi ya wanaume ambao Amber Ray amewahi kuchumbiana nao

Amber Ray anafahamika kuwahi kuwa kwenye mahusiano na zaidi ya wanaume kumi

Muhtasari

•Mama huyo wa mtoto mmoja anafahamika kuwahi kuwa kwenye mahusiano na zaidi ya wanaume kumi.

Amber Ray
Image: Hisani

Amber Ray ni mwanasoshalaiti ambaye anajulikana kutochoka ifikapo ni suala la kutafuta mapenzi.

Mama huyo wa mtoto mmoja anafahamika kuwahi kuwa kwenye mahusiano na zaidi ya wanaume kumi.

Hawa hapa baadhi yao:-

1. Jimal Marlow

Amber Ray alimtambulisha Mwenyekiti wa Chama cha waendeshaji Matatu Jamal Rohosafi kama mpenzi wake mpya baada ya miezi kadhaa ya uvumi mtandaoni.

Sosholaiti huyo aliweka uhusiano wao hadharani baada ya kurekodiwa kwa siri mara kadhaa na picha zao kusambazwa mtandaoni.

Jamal baadaye, katika mahojiano na Jalang’o, alithibitisha kwamba Amber Ray ni mpenzi wake licha ya kuwa alikuwa kwa ndoa na watoto wawili.

Alisimulia mwingiliano wake wa kwanza na sosholaiti huyo na akadai kwamba ‘alimwiba’ kutoka kwa mke wake wa kwanza.

"Kuna uvumi mwingi kwamba Amber aliniibia kutoka kwa mke wangu,lakini watu wanasahau kuwa nilikuwa kondakta, ambayo inamaanisha najua jinsi ya kutongoza wanawake," Jamal alisema.

Sosholaiti huyo baadaye aliachana na Jamal kisha bosi huyo wa Matatu akarudi kwa mkewe.

2. Amber Ray na Kabba

Kufuatia kutengana kwake na Jamal Rohosafi, Amber Ray aliendelea na mchezaji wa mpira wa vikapu wa Sierra Leone aliyejulikana tu kama Ib Kabba.

Wawili hao walisherehekea mahusano yao hadi walipoanza kubishana juu ya picha, Kabba  alionekana kutoridhishwa na aina ya picha ambazo sosholaiti huyo alikuwa anachapisha kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumzia kuhusu kuachana kwao, mwanariadha huyo alieleza kuwa aliachana na Amber Ray kwa kuwa hakuwa tayari kuwa mke, na kuongeza kuwa hatawahi chumbiana na mwanamke wa Kambaland.

"Nashangaa kwa nini watu wengi huko nje wanafikiri kuwa ni wanaume pekee wanaotumia wanawake, wanawake ni hatari sana sanan Kambaland ni sehemu ambayo sitatamani kutembelea maishani mwangu'' Mwanariadha huyo alisema.

3. Brown Mauzo

Miezi michache kabla ya kuingia kwenye uhusiano mpya na Jamal, mrembo huyo alichumbiana na mwanamuziki maarufu Fredrick Kilonzo Mutinda almaarufu Brown Mauzo.

Wawili hao walitimiza malengo ya wanandoa kutoka 2019 hadi kutengana mnamo Januari 2020.

4.Zaheer Merlahi Jhanda

Amber pia alichumbiana na mwanasiasa mashuhuri Zaheer Merlahi Jhanda na walionekana kuwa watulivu na wasioweza kutenganishwa.

Mnamo Agosti 2018, alijitokeza hadharani kutangaza kwamba alikuwa ametengana na Zaheer.

5. Syd

Bila kujipa muda wa kupona kutokana na kutengana kwake hapo awali, Amber alianza kushirikiana na rapa na promota maarufu Syd mapema mwaka wa 2018.

Wawili hao walichumbiana kwa miezi michache tu kabla ya kuachana na mpango huo mnamo Desemba 2018.

6. Baba Gavin

Hapo zamani Amber alichumbiana na mtu wa ajabu ambaye walizaa naye mtoto wa kiume. Wawili hao waliachana na kukubaliana kumlea mtoto wao wa kiume.

Hakuna anayejua jina kamili ya babake mtoto lakini uvumi umeenea kwamba yeye ni mtu maarufu nchini Kenya.

7. Kenny Rapudo

Kwa sasa Amber Ray anachumbiana na mfanyabiashara Kenny Rapudo. Hakuna mengi yanayojulikana kuhusu mfanyabiashara ambaye ameonekana akichukizwa na sosholaiti mara kadhaa.

Rapudo pia amekuwa akiandamana na sosholaiti kwenye hafla za kijamii.