Ommy Dimpoz afunguka alivyowekewa sumu nusura apoteze uhai

Dimpoz alikosekana kwenye sanaa kwa takriban miaka mitatu.

Muhtasari

•Baada ya tukio hilo lilitokea 2018 Dimpoz alibaki akipambania uhai wake huku akifanyiwa oparesheni tatu maalum za koo katika juhudi za kuokoa maisha yake.

Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz
Image: INSTAGRAM

Staa wa muziki Ommy Dimpoz amefunguka mbele ya mashabiki wake jinsi aliwahi kuwekewa sumu nusura apoteze uhai.

Baada ya tukio hilo lilitokea 2018 Dimpoz alibaki akipambania uhai wake huku akifanyiwa oparesheni tatu maalum za koo katika juhudi za kuokoa maisha yake.

Jumapili wakati akitumbuiza katika kipindi cha 'Break Point', Dimpoz aliimba "Sumu Waliniwekea, Bado Nusu Nikufuate Mama."

Hii inatafsiriwa kwamba  kwa sasa angekuwa marehemu, kwani ilibaki kidogo amfuate mama yake ambaye alitangulia.

Ommy Dimpoz ambaye ameuanza vyema mwaka huu huku tayari akiwa ameachia ngoma mbili, aliwahi kufichua kuwa tatizo la  koo lake lilitokana na sumu. 

Katika mahojiano na Millard Ayo, Ommy alifichua kwamba sauti yake ilirudi kabla ya kupelekwa nchini Ujerumani ambako alifanyiwa oparesheni ya tatu na ya mwisho.

Ikumbukwe, ni takribani miaka mitatu sasa imepita Dimpoz hakuonekana jukwaani akitumbuiza.

Jumapili Dimpoz alifanya tamasha yake ya pili ya  "Cheusi Cheupe" katika viwanja vya Zakhem, Mbagala jijini Dar es salaam.

Alishinda tuzo ya wimbo bora wa Kushirikiana mwakani 2012 kufuatia kibao alichoshirikisha  Ali Kiba.

Alianza kuimba akiwa shule ya msingi, lakini alipata tu kutunga wimbo wake wa kwanza alipokuwa shule ya upili.