(Video) Zuchu aweka urembo wa meno, pete kubwa kama Diamond, wambea wasema haya

Zuchu na Diamond wamekuwa wakisemekana kuwa katika mahusiano ya kimapenzi.

Muhtasari

• Zuchu amekuwa akibanwa sana katika mahojiano kwa maswali ya uwepo wa mahusiano yao lakini amekuwa akiguna kuwa ni kazi tu hakuna mahusiano.

Msanii pekee wa kike katika rekodi lebo kubwa kabisa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, WCB Wasafi, Zuchu amelisukuma gumzo la uwepo wa mahusiano baina yake na bosi wake Diamond Platnumz mbele baada ya kupakia picha zake akiwa amemuiga Diamond katika mitindo yake.

Kupitia ukurasa wake wac Instagram, Zuchu alipakia picha na video akionesha jinsi ambavyo amemuiga Diamond kuweka urembo katika meno yake pamoja na pete za kimapambo, pete moja kubwa kwenye kidole cha mwisho cha mkono wa kulia, kama ambavyo Diamond anavaa.

Msanii huyo ambaye yupo nchini Afrika Kusini kuandaa video ya ngoma alizua gumzo kali kutokana na uigaji huo kwa bosi wake na kufanya wengi waamini kwamba wawili hao wapo katika mahusiano, uvumi ambao umekuwa ukizungumziwa sana kwa muda mrefu sasa.

“Hapa sasa ni tabasamu zuri tu. Ahsante sana Diamond Platnumz,” Zuchu alifuatisha picha hizo na maneno hayo yaliyoonekana kwamba anamshukuru bosi wake kwa kumfunza mbinu hizo za kujiremba ambazo kwa muda mrefu zimekuwa ni za Diamond tu mpaka kuwa kama nembo ya utambulisho wake.

Wambea walizuka kwenye picha hizo alizozipakia Jumamosi asubuhi na kuachia yao ya moyoni ambapo walisema sasa dhibitisho tosha kwamab wawili hao wamepanga kuigana hadi uvaaji maanake wao ni mwili mmoja kimtindo.

Zuchu na Diamond kwa muda mrefu wamekuwa wakisemwa kuwa wapo katika mahusiano japokuwa hakuna hata mmoja baina yao amekiri wazi wala kukataa bayana uwepo wa mahusiano yao.

Zuchu amekuwa akibanwa sana katika mahojiano kwa maswali ya uwepo wa mahusiano yao lakini amekuwa akiguna na kumalizia kwamba anamchukulia Diamond kaam bosi wake kimuziki.

Kwa upande wake Diamond amekuwa akiulizwa ambapo waakti mmoja wakiwa kweney mahojiano na pamoja na Zuchu, mwanadada huyo aliulizwa swali la kuchumbiana na Diamond lakini Simba akadakia kwa haraka na kumkatiza huku akisemac kwamba maswali kaam hayo ni ya ukakasi na ndio maana alimsaidia Zuchu kujibu ili asije akazungumza mambo yasiyofaa.

Familia nzima ya WCB Wasafi imekuwa ikilikwepa suala hilo ambalo mpaka sasa chawa Baba Levo pekee ndiye anaonekana kuzungumza tena kwa kunadi kwamba Mondi na Zuchu ni wapenzi japo maneno yake yanachukuliwa kimzaha.