Kila sekunde iendayo kwa Mungu, dunia huwapa watu wake mambo mapya, mengine ya kustaajabisha, kuogofya, kutisha na mengine ya kukosha na kufurahisha.
Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 65 amearifiwa kumuoa mamake wa kambo pindi babake mzazi alipofariki.
Kulingana na video moja iliyopakiwa kweney jukwaa la YouTube na mkuza maudhui mmoja, anaeleza kwamba mwanaume huyo kwa jina Umweze alipatwa na hisia za kimapenzi na mamake wa kambo kwa jina Nabusane, na wote walijenga hisia zao kimapenzi pindi baada ya mume wa Nabusane ambaye ni babake Umweze kufariki.
Katika video hiyo, Msimulizi anaeleza kwamba babake Umweze alioa mwanamke huyo baada ya mkewe wa kwanza kufariki na wakaishi kwa ndoa kwa miaka miwili kabla ya mzee mwenyewe kutangulia mbele za haki pia kumfuata mkewe wa kwanza ambaye ni mamake Umweze.
Baada ya kifo cha mzee, mwanaume huyo alibaki nyumbani na mamake wa kambo ambapo waliishi kwa muda peke yao, jambo ambalo linakisiwa ndilo chanzo cha hisia za mapenzi kuota baina yao.
Baada ya kugundulika kwamab wameingia katika mapenzi na mamake wa kambo, jamii iliwasuta vikali lakini mwanaume huyo alisema kwamba hajutii hata chembe kwani mapenzi yake na mamake wa kambo ni ya kudumu.
Msimulizi anasema kwamba mwanaume huyo aliwafuata wazazi wa mamake wa kambo na kuwaeleza nia yake ya kumuoa na kumfanya mkewe jambo ambalo lilipokelewa kwa mshtuko mkubwa ila mwisho wa siku wakamkubalia kutoa mahari, sharti ambalo alitekeleza na kukubaliwa kuishi na mamake wa kambo kama mkewe.
Hii hapa ni simulizi yenyewe!