logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Karua amblock Twitter mwanadada aliyeshiriki mchango wake, sahani ya chakula 50K

“Mbona mambo mabaya hutendeka kwa watu wazuri? Sio jambo la kuzua mzaha bana na hicho chakula cha jioni kilikuwa sahani ni 50K,” - Mabeya

image
na Radio Jambo

Makala11 September 2022 - 12:59

Muhtasari


• Karua aliandaa chakula cha jioni mnamo mwezi Mei mwaak huu kuchangisha pesa za kampeni, sahani ilikuwa inaenda kwa 50K.

Damaris mabeya alilalama hatua ya Martha Karua kumblock Twitter

Mjasiriamali na mwasisi wa shirika la kutetea haki za mtoto wa kina la Aminia Dada Damaris Mabeya amesikitishwa baada ya kugundua kwamab aliyekuwa rafiki wake na mgombea mwenza wa Azimio One Kenya Martha Karua alimpiga ‘block’ kwenye Twitter.

Mabeya alipakia picha za kudhibitisha hilo na kushangaa hajui ni nini kilitokea kati yake na Karua mpaka kufungiwa kutoona kile ambacho mwanasiasa huyo anafanya kwenye mtandao wa Twitter.

Mabeya alidokeza kwamba alikuwa ni mtu wa karibu sana na Karua na hadi alishiriki hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Karua ili kuchangisha fedha za kufahdili kampeni za Azimio mnamo mwezi Mei mwaka huu, hafla ambayo chakula sahani moja kilikuwa kinauzwa kwa shilingi elfu 50 pesa za benki kuu ya Kenya.

“Jinsi ilianza nilipoenda kwa chakula cha jioni cha Martha Karua na jinsi inaendelea sasa,” Mabeya aliandiak huku akifuatisha udhibitisho kwamba kweli Karua amemlisha ‘block’ kwenye Twitter.

Watu wengi walicheka huku wengine wakimuambia kwamba huenda alijipata katika hali hiyo baada ya pengine kuandika kitu cha kumkejeli Karua baada ya Azimio kupoteza kura na pia kesi waliyopeleka mahakama ya upeo kutaka kubatilishwa kwa ushindi wa Ruto.

“Mbona mambo mabaya hutendeka kwa watu wazuri? Sio jambo la kuzua mzaha bana na hicho chakula cha jioni kilikuwa sahani ni nusu laki,” Mabeya aliandika kuwajibu wale waliokuwa wakimchekelea.

Wengine walisema mwanasiasa huyo aliyebatizwa jina la Mama bila mchezo amefungia watu wengi kutoona akaunti yake ya Twitter kutokana na kumkejeli.

“Akaunti ambazo Karua amefungia Twitter ni nyingi kuliko zile kura alizolea Azimio,” Mmoja alizua utani wa kejeli.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved