logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tunatumia mswaki mmoja na mpenzi wangu- Dorea Chege

Muigizaji huyo amefichua kuwa huwa anavaa nguo za mpenziwe zikiwemo chupi.

image
na

Dakia-udaku22 September 2022 - 05:28

Muhtasari


• Dorea Chege alimtambulisha mpenzi wake Dj Dibul kwenye mtandao mwezi wa Julai.

• Dorea Chege aliwania kiti cha mwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi kama mgombea huru na kupoteza.

Muigizaji Dorea Chege almaarufu Maggie Maria amefichua mambo ya kushangaza katika mahusiano yake na  Dj Dibul.

 Dorea ambaye alikuwa akiigiza katika kipindi cha Maria amekuwa akiishi pamoja na mpenziwe DJ Dibul kwa muda sasa na wamekuwa wakitumia mswaki mmoja  miongoni mwa vitu vingine vya kibinafsi  pamoja.

Dorea amefichua kuwa huwa anavaa nguo za mpenziwe zikiwemo chupi na kutumia vitu vingine kama mswaki wa mwenzake.

“Dj Dibul hubadilisha mswaki wake kila wiki, ila tunatumia mswaki mmoja, mimi hutumia wake na yeye hutumia wangu,”alisema.

Muigizaji huyo alimtambulisha mpenziwe Dj Dibul kupitia mitandao ya kijamii mwezi Julai ila hawajaeleza lini walijipata kwenye lindi la mahaba.

Walifichua kuwa walijua wanapendana walipopanga  date yao kwanza na kujipata kila mmoja amevutiwa na mwingine. Wapenzi hao wamepanga kuendeleza  uhusiano wao kwa lengo la kuanzisha familia pamoja.

Dorea alisema angetaka kuwa na mtoto mmoja ila mpenzi wake Dj Dibul alipinga na kusema angetaka watoto wannne, wasichana wawili na wavulana wawili.

Dorea Chege alifichua kwamba kama hangekuwa kwenye uhusiano na Dibul angekuwa ameolewa kwingine na hadi kupata uja uzito.

Muigizaji huyo alipata umaarufu zaidi wakati akiigiza katika Kipindi cha Maria kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Citizen mwaka jana.

Dorea amekuwa akiwakosesha wanaume wengi usingizi kutokana na urembo wake na picha ambazo amekuwa akipakia mitandaoni.

Hivi majuzi Dorea Chege alikuwa akiwania kiti cha mwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi kama mgombea huru.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved