logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ Mo atokea ghafla kwenye mahubiri ya mkewe Size 8

"Mko salama, mmebarikiwa? Nimekujia mke wangu amkeaa huku siku tatu nimpeleke nyumbani," DJ Mo alisema.

image
na Radio Jambo

Makala03 October 2022 - 12:54

Muhtasari


• Size 8 alikuwa Kibwezi ambako walikuwa wameandaa tamasha la mahubiri  ya siku 3 wakiwa na wahubiri wenzake.

• Tamasha hilo lilihudhuriwa na waumini wengi waliokuwa wanaomba na kusikiliza mahubiri.

Wanandoa Size 8 na mumewe DJ Mo wanasemekana kuvunja ndoa yao

Samuel Muraya almaarufu Dj Mo alimpa mkewe Size 8 bonge la shtukizi katika tamasha moja la mahubiri Size 8 alikuwa anahubiri huko Kibwezi kaunti ya Makueni.

Dj Mo hakuwa ametarajiwa kutokea katika tamasha hilo la mahubiri na alitokea ghafla kumuunga mkewe mkono akifanya mahubiri. 

Mchungaji Size 8 alikuwa amekita kambi za mahubiri katika kaunti hiyo ya Makueni kwa siku tatu kueneza injili.

"Mko salama, mmebarikiwa? Nimekujia mke wangu amkeaa huku siku tatu nimpeleke nyumbani," DJ Mo alisema baada ya kutokea ukumbini ghafla kama chafya.

Size 8 alikuwa Kibwezi ambako walikuwa wameandaa tamasha la mahubiri  ya siku 3 wakiwa na wahubiri wenzake.Tamasha hilo lilihudhuriwa na waumini wengi waliokuwa wanaomba na kusikiliza mahubiri.

Katika tamasha hilo walilokuwa wamandaa ya siku tatu, video ya Size 8 akitoa mapepo na kuomba ilienea mitandaoni .

Alikuwa anayaombea mapepo yaweze kumtoka mwanadada ambaye alikuwa na roho ya uovu ndani yake .

"Ako na pepo linatembea kwa mwili wake, linatoka kwa kichwa ilnazunguka . Na asubuhi nilipokua nikiomba Yesu aliniambia anakuja kutoa wafungwa kwa mifungo za shetani katika jina la Yesu. Wewe pepo hauna mamlaka,mamlaka ni ya Yesu. Sasa wewe peopo nakukemea utoke katika jina la Yesu," aliomba Size 8 akiwa kwenye mahubiri yake.

Baadaye Siz 8 alimwambia mwanadada huyo kuwa ako huru wa pepo hilo

Mwanamuziki huyo alitawazwa kama mhubiri mwaka jana akiwa kwenye maombi baada ya kuokoka kwa miaka kadhaa na pia kufuzu katika taaluma ya uchungaji.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved