logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bintiye Sonko awasuta wanamitandao wanaokejeli muonekano mpya wa Vera Sidika

Sandra ameeleza kutoridhishwa kwake na kejeli nyingi ambazo mwanasoshalaiti huyo amepokea.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 October 2022 - 06:47

Muhtasari


  • •Sandra Mbuvi amewasuta wanamitandao wanaomfanyia matani na kumkejeli mwanasoshalaiti Vera Sidika kwa kufanya mabadiliko ya mwili yaliyomuacha na makalio madogo.
  • •Sandra aliwashauri wanamitandao kuacha kukejeli watu ambao hawajawakosea kwa jambo lolote kutokana na wasiwasi wao wenyewe.

Bintiye Sonko, Sandra Mbuvi amewasuta wanamitandao wanaomfanyia matani na kumkejeli mwanasoshalaiti Vera Sidika kwa kufanya mabadiliko ya mwili yaliyomuacha na makalio madogo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sandra ameeleza kutoridhishwa kwake na kejeli nyingi ambazo mwanasoshalaiti huyo amepokea tangu alipofichua muonekano wake mpya siku ya Jumatano. 

Alihoji kwa nini wanamitandao walikuwa wakimhukumu mwanasoshalaiti huyo alipokuwa na makalio makubwa na pia  sasa wakati  ambapo amefanyiwa upasuaji wa marekebisho ya kurejesha makalio asili.

"Mbona mnachukulia kila jambo vibaya na kuona baya katika kila kitu? Inaudhi sana .Mlikuwa mnamhukumu Sidika alipokuwa na makalio makubwa kwa kuwa hakuwa na makalio asili na kuwa alikuwa amefanyiwa upasuaji ili kuyaongeza ila sasa ambapo ameamua kuwa na makalio asili na kufanyiwa upasuaji ili kutoa yale bandia mnamkejeli na kumshambulia kwa maneno mitandaoni," alisema.

Mfanyabiashara huyo ambaye alionekana kutopendezwa na maoni ya watu ambao walitafuta jambo lolote ili kumkejeli Sidika alibainisha kuwa hata  mke huyo wa Brown Mauzo awe na umbo lipi wanamitandao hawataridhika.

Sandra aliwashauri wanamitandao kuacha kukejeli watu ambao hawajawakosea kwa jambo lolote kutokana na wasiwasi wao wenyewe.

"Acheni kuonyesha wasiwasi wenu kwa watu wengine wasiowahusu na ambao watashinda na kufaulu mwishowe wa siku," mfanyibiashara huyo aliwafokea watu.

Hii ni baada ya Sidika kuanika picha yake mtandaoni iliyoonyesha upungufu wa makalio yake na kusema kuwa alifanyiwa upasuaji wa makalio ili kuyapunguza kutokana na sababu za kiafya.

Wanamitandao wamekuwa wakitoa hisia mseto baada ya mwasoshalaiti huyo kuonyesha mabadiliko makubwa ya mwili wake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved