logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize na Kajala wachorwa tattoo kwa mara ya pili baada ya kurudiana

Wawili hao walitoa tattoo walizokuwa nazo hapo mwanzo kabla ya kuachana mwaka jana.

image
na Radio Jambo

Burudani12 October 2022 - 08:30

Muhtasari


• Walikuwa wameweka tattoo kama sasa ila walikuwa wameongeza taji juu ya herufi zao na ishara za kushiria mapenzi yao, ila Kajala alikuwa amechorwa herufi H kuashiria jina la mwanamuziki huyo la kibiashara,

• Baada ya kuachana, Harmonize alichorwa tattoo nyingine kwenye mguu wake ya mpenzi wake Kajala akiwa na mwanawe Paula.

Mwigizaji Kajala amepakia video inayoonyesha kuwa yeye na mwanamuziki Harmonize wamechorwa tattoo kwenye vidole vyao vya pete.

Wawili hao waliwajulisha mashabiki wao kuhusu tukio hilo jipya kwenye uhusiano wao kupitia ukurasa wa Kajala wa Instagram.

Harmonize na Kajala walikuwa wamewahi kuweka tattoo za herufi zao hapo awali kabla ya kuachana, Kajala akiwa amechorwa herufi R huku Harmonize akiwa amechorwa herufi K.

Walikuwa wameweka tattoo kama sasa ila walikuwa wameongeza taji juu ya herufi zao na ishara za kushiria mapenzi yao, ila Kajala alikuwa amechorwa herufi H kuashiria jina la mwanamuziki huyo la kibiashara,

Walipoachana mwaka jana, wote walifuta tattoo hizo na kuzirekebisha kwa kubadilisha mauombo na kuweka mengine.

Baada ya kuachana,Harmonize alichorwa tattoo nyingine kwenye mguu wake ya mpenzi wake Kajala akiwa na mwanawe Paula.

Alisema kuwa alichora tattoo hiyo kama ishara ya kumwomba msamaha Kajala kwa yale yote aliyokosea walipokuwa kwenye uhusiano wakati huo.

"Hakuna ambacho kitabadilisha kuwa nilikosea familia yangu. Hakuna ambacho kitabadilisha kuwa ni familia yangu. Pia hakuna ambacho kitabadilisha kuwa najivunia familia yangu Mguu Wangu wa kulia utasema Sorry mpaka Siku Yangu Ya Mwisho," Harmonize alisema akiomba msamaha.

Uhusiano wao umekumbwa na changamoto nyingi ikiwemo kilichosababisha wao kuachana wakati huo na Kajala kuendelea na maisha yake.

Wawili hao walikuwa wameachana kwa kuwa Harmonize alikuwa amemtumia bintiye Kajala,Paula picha zake akiwa uchi.

Baada ya hapo, mpenzi huyo wa Kajala alikuwa na majuto kwa kufanya hayo na alilazimika kumwomba Kajala msamaha kwa aliyofanya.

Harmonize alifanya mambo ya kusisimua kama kumnunuilia gari Kajala, aina ya Range Rover na pia aliweka bango barabarani ili Kajala amsamehe.

Pia, alimnunulia mwigizaji huyo mkufu wa thamani  na kutundika picha yake katika chumba chake cha kulala.

Hata baada ya kurudiana, mtangazaji Mwijakau amedai kuwa Harmonize ako kwenye mahusiano na Kajala na bintiye Paula kwa wakati mmoja.

Mtangazaji huyo alisema kuwa ana ushahidi wa kutetea alichokuwa akidai kwa kuwa amewahi kuitembelea familia hiyo na kuona kilichokuwa kinaendelea na alichokuwa akifanyiwa Paula.

Siku moja nilienda kwa Harmonize nikamkuta sebuleni amekaa na Boxer halafu Paula anampapasa kifuani mimi kama Mzazi sikupenda nikamwambia hii sio sawa akaniambia haya ni mambo ya kifamilia yaache, akasema Pesa inaoongea,” Mwijaku alisema.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved