logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtahiniwa wa kidato cha 4 afariki wiki chache kuelekea mitihani ya kitaifa

Mtahniwa huyo alikufa maji alipoanguka kwenye maporomoko ya mji walipokuwa wamezuru Mlima Kenya.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 November 2022 - 14:21

Muhtasari


  • • Mwanafunzi huyo alizikwa kaunti ya Kirinyanga huku wazazi na majirani wakionyesha huzuni yao kutokana na kifo cha msichana huyo mchanga.
Mwanafunzi wa Mugoiri girl azikwa.

Wingu la simanzi na majuto lilitanda kwenye mioyo ya wanafunzi wa kidato cha nne baada ya mmoja wao kuzikwa mnamo Novemba 14.

Mwanafunzi huyo alizikwa kaunti ya Kirinyanga huku wazazi na majirani wakionyesha huzuni yao kutokana na kifo cha msichana huyo mchanga.

Mwanafunzi huyo, Grace Wanjiku alifariki kwenye maporomoko ya maji kwenye mto wa Kathitha walipokuwa wamezuru mlima Kenya kwa ziara ya shule kama njia moja ya kujifurahisha kabla ya mtihani wao wa kidato cha nne kuanza.

Kwenye video ambayo ilipakuliwa kwenye mtandao ya Tiktok ulionyesha waombolezaji wakiwa wanahuzunika na wengi wakiwa wamefika kumpa mkono wa burini msichana huyo.

Kifo cha mwanafunzi huyo kinaendela kuzua hisia nzito kutoka kwa Wakenya kuhusiana na usalama wa wanafunzi wakiwa shuleni kwani wanaamini tukio hili lingeepukika na familia yake Grace haingeishi kwa majuto ya kumpoteza mwanao ambaye pengine angewasaidia kwenye siku za usoni.

Inahuzunisha sana ikionekana mwanafunzi huyo alifariki wiki tatu kabla ya kufanyika kwa mtihani wa kidato cha nne ambao unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Hisia za kuhuzunisha ziliandikwa kwenye mtandao wa tiktok huku wanamitandao wakiungana na familia kutoa rambirambi zao na kuwaombea Mungu awape nguvu nyakati hizi za kupoteza mpendwa wao.

''Makiwa familia nzima. inasikitisha kumwona msichana huyo mchanga amekufa'' mmoja mtumizi wa mitandao aliandika.

''Mungu awafariji wazazi na wanafunzi wa Mugoiri. Mkasa huo hauwezi elezeka kwa maneno'' mwingne aliandika


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved