logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Muuzaji akanganya wanunuzi, atangaza bei ya mayai na kusema hataki sarafu

Katika tangazo hilo, alisema anauza yai moja shilingi 13 lakini akatoa ilani kuwa hachukui sarafu.

image
na Radio Jambo

Habari19 November 2022 - 07:51

Muhtasari


• “Mayai ni 13/=, shilingi sichukui!” Ujumbe huo unasoma.

Picha moja ya muuzaji akipakia tangazo la bei mpya za biashara yake ya mayai imezua mjadala mitandaoni kwa ukanganyaji mkubwa.

Kulingana na maandishi kwenye bango hilo lililoweka pembezoni mwa trei la mayai, mfanyibiashara anaachia ujumbe unaosoma kuwa yai moja linakwenda kwa shilingi 13 pesa za Kenya, hapo sawa!

Kinachowachanganya wengi ni mwendelezo wa tangazo hilo ambao unaonekana kuwa tahadhari kwa wanunuzi wote ambapo anawaambia kuwa hawezi kupokea shilingi bali anataka sarafu moja iwe ni 10 au 15 basi.

“Mayai ni 13/=, shilingi sichukui!” Ujumbe huo unasoma.

Kwa haraka haraka kufafanua ni kwamba mfanyibiashara huyo anauza mayai kwa shilingi 13 lakini hataki sarafu za shilingi moja moja kati ya 10 na 15 bali anataka kiwango sawa. Kwa mfano ukienda kununua ni labda uende na shilingi 10 ikiwa moja au shilingi 15 ikiwa ni sarafu ya 10 na ile ya shilingi 5.

Picha hiyo iliibua mjadala mitandaoni ambapo baadhi waliitafsiri kivyao huku wengine wakishindwa kuelewa ni nini haswa mfanyibiashara huyo alikuwa anamaanisha.

“Huu ni uendawazimu kwa kweli,” mtumizi mmoja kwa jina Kijana ya Atwoli alisema.

“Huyo anataka kuwafukuza wale wa kununua moja, anataka mtu wa kununua mayai matatu unatoa shilingi 40, shilingi moja inabaki naye kama msaada kwa shirika la msalaba mwekundu,” mwingine alitania.

“Hapo mimi nanunua mayai mawili halafu nampa noti ya elfu moja naye ataabike kunitafutia salio langu,” Kahit Kashmil alisema.

Je, wewe unaelewa nini na tangazo hili la bei ya mayai kwa mdau?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved