logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(screenshot) Amira ajibu madai ya Jimal kwamba hakuwa mjamzito miaka 2 iliyopita

Amira hatimaye ametoa barua ya hospitali na kipimo ambacho kilionyesha kuwa mjamzito.

image
na Radio Jambo

Makala08 March 2023 - 14:44

Muhtasari


  • Alisema kuwa Amira amejitosa katika kuharibu jina lake kwa madai ya uwongo kwani ameacha kumlipa kodi ya nyumba

Baada ya madai ya Mwenyekiti wa Muungano wa Wamiliki wa Matatu jijini Nairobi, Jimal Marlow Rohosafi kukana madai ya aliyekuwa mke wake, Amira kwamba takriban miaka miwili iliyopita aliwahi kumpiga vibaya hadi kumfanya apoteze mimba.

Amira hatimaye ametoa barua ya hospitali na kipimo ambacho kilionyesha kuwa mjamzito.

Kwenye mahojiano ya kipekee na Mpasho, Jimal alidai kwamba mama huyo wa watoto wake wawili hata hakuwa katika nafasi ya kuweza kubeba ujauzito katika kipindi ambacho anadai kuwa alimpiga.

Mfanyibiashara huyo mashuhuri alifichua kwamba walikuwa wamekubaliana kutopata watoto wengine kwani Amira ana tatizo la mgongo ambalo linafanya iwe ngumu kwake kubeba ujauzito.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Amira alisema;

"Nimetoka kutazama mahojiano sasa hivi, wacha ata mimi nitoe kadi yangu, huyu mwanamume alisema kwamba sikuwa mjamzito,huu hapa baadhi ya ukweli,"Aliandika Amira.

Jimal alibainisha kuwa hakuna jinsi angeweza kumpiga mama huyo wa watoto wake akiwa mjamzito, na mbele ya watu.Pia alibainisha kuwa umma ungejua kwa uhakika kama angekuwa na ujauzito kama anavyodai.

Alisema kuwa Amira amejitosa katika kuharibu jina lake kwa madai ya uwongo kwani ameacha kumlipa kodi ya nyumba.

"Niliacha kumpatia pesa ya matumizi wiki mbili zilizopita. Nilimwambia kuwa siwezi kuendelea kumpatia pesa ya matumizi kwa sababu nakaa na watoto na yeye pia anakaa na wao. Ni asilimia hamsini hamsini," alisema.

Mnamo siku ya Jumatatu, Wakati Amira akiwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram alimshtumu mume huyo wake wa zamani  kwa kuwa mtu mkatili.

Hizi hapa picha ambazo Amira alipakia kwenye ukurasa wake wa instagram;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved