Jimal Rohosafi wamkaribisha mwana wao na Michelle Wangari

Jimal alitangaza ujauzito wa Michelle siku ya wapendanao.

Muhtasari

• Jimal alitangaza habari hizo kwa mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa.

Image: INSTAGRAM// JIMAL ROHOSAFI NA MICHELLE WANGARI

Mfanyibiashara Jamal Marlow, almaarufu Jimal Rohosafi, amemkaribisha mtoto na mpenziwe, Michelle Thiong'o.

Walimkaribisha mwana wao ambaye ni binti kwa jina Amal J.Ibrahim.

Jimal ni mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Matatu na pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma Credit. Amal ni mtoto wake wa kwanza na Michelle

Jimal alitangaza habari hizo kwa mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii mnamo siku ya Ijumaa.

"Nina madoa mengi si mkamilifu ila nina baraka nyingi kutokuwa na shukrani,"alichapisha Jimal kwenye Instagram.

Michelle pia alieleza furaha yake mtandaoni, 'Singependa namna ingine,"aliandika Michelle

Hapo awali, Jimal alisema Michelle ana sifa za mwanamke ambaye alikuwa akimtafuta.

Jimal aliachwa na wake zake wawili, Amira na Amber Ray mwaka jana.

Amira alitangaza kuwa aliwasilisha maombi ya talaka kwa 'kukosa heshima' huku Amber akisema uhusiano wake na Jimal ulikuwa umeisha.

Jimal alisema kwamba alikuwa amechumbiana na Michelle kwa mwaka mmoja.

"Tulianza uchumba siku ya wapendanao 2022. Alikuwa mfanyakazi wangu lakini kabla ya hapo alikuwa rafiki yangu na tulikuwa tukipiga soga sana," alisema.

Jimal alisema alivutiwa naye baada ya kujua kwamba alikuwa amefanya kozi ya usimamizi wa fedha.

Iliposemekana kuwa wawili hao walikuwa wakichumbiana, Jimal alimwomba aliyekuwa mke wake Amira amsamehe lakini alikataa, licha ya yeye kumsihi mtandaoni.

Amira alisema msamaha ulimrudisha katika mojawapo ya nyakati zenye giza sana maishani mwake kwani aliteseka sana baada ya kukosewa heshima.

"Ni nzito, siwezi kuielewa kwa sasa lakini namuomba Mwenyezi Mungu anipe neema. Vidonda vingine haviponi, lazima ujifunze jinsi ya kuishi navyo."

Jimal alisema dini yake inamruhusu kuoa wake wanne.

"Nilipoomba msamaha, nilikuwa nachumbiana, ni nini kikubwa? Ni sehemu ya dini yangu na hakuna dhambi huko," alisema.

"Naweza kuoa leo, kesho na sio shida mradi tu nitaweza."

Jimal ameahidi kuwapa mashabiki wake chai zaidi mnamo 2023.