logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Karen Nyamu amliwaza Omanga baada ya video chafu inayodaiwa kuwa yake kusambazwa

Seneta Nyamu alibainisha kuwa hakuna chochote cha kuonea aibu pale.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri18 April 2023 - 05:40

Muhtasari


•Karen Nyamu amempa pole Millicent Omanga baada ya video inayodaiwa kuwa ya uchi wake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

•"Shenzi kabisa wewe. Kwa hakika nimeskia wakisema anakaa fiti sana. Weka kichwa chako juu Mhe Millicent Omanga" Karen alisema.

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu amempa pole mwanasiasa mwenzake, Millicent Omanga baada ya video inayodaiwa kuwa ya uchi wake kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii siku ya Jumatatu.

Video ya mwanamke aliye uchi iliyorekodiwa wakati usiothibitishwa ilisambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya Wakenya wakidai mhusika ni CAS huyo. Walakini, hakuna kilichothibishwa kufikia sasa.

Akizungumza kuhusu video hiyo, seneta Karen Nyamu alibainisha kuwa hakuna chochote cha kuonea aibu pale.

"Hakuna cha aibu kabisa hapo. Sote tumekuwa tukilala uchi wakati fulani, kuna shida gani! Ni lazima umakini uondoke kutoka kwa mwanamke hadi kwa mpumbavu aliyechukua video hiyo. Kwani wewe ni mtoto? Nia yako ni nini?," Nyamu alisema kupitia ukurasa wake maarufu wa mtandao wa Facebook.

Seneta huyo hata hivyo alibainisha kwamba CAS Omanga ni mwanamke jasiri ambaye hawezi kuyumbishwa na jambo kama hilo. Aliendelea kumkosoa mtu aliyerekodi video hiyo na kuhoji kuhusu nia yake.

"Shenzi kabisa wewe. Kwa hakika nimeskia wakisema anakaa fiti sana. Weka kichwa chako juu Mhe Millicent Omanga" alisema.

Jumanne asubuhi, Waziri msaidizi mteule katika wizara ya usalama wa ndani Millicent Omanga alivunja kimya baada ya kile kinachodaiwa kuwa video yake ya utupu kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, Omanga alinukuu Bilbia yenye kifungo cha kujiliwaza ambapo Mungu anawaambia waja wake kwamba amewapa nguvu na hakuna kitakachowaumiza.

“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru." Luka 10:19. Siku njema wadau,” aliandika.

Hata hivyo, haijabainika iwapo ni kweli video hiyo inayoenezwa ikimuonesha mwanamke akiwa nusu uchi ni Omanga ama ni watu tu wenye nia mbaya waliamua kufanya uhariri kuonyesha kama kwamba ni yeye.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved