logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Davido adaiwa kuachwa na mkewe kwa kupata mtoto mwingine na baby mama wake

Kuna madai zaidi kwamba Davido alijaribu kumpa mwanamke huyo shinikizo la kutoa mimba hiyo.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani21 April 2023 - 10:48

Muhtasari


  • •Mwanamke huyo anaishi Atlanta, Marekani ambako Davido amekuwa akitembea mara kwa mara katika ziara zake za Marekani.
  • •Chanzo sasa kinadai Amanda tayari amejifungua mtoto, na Chioma amemuacha Davido kwa mara nyingine tena

Mwimbaji David Adedeji Adeleke, anayejulikana kitaaluma kama Davido, anavuma mtandaoni. Anadaiwa kumpa ujauzito mpenzi wake mwingine anayeitwa Amanda anayeishi Marekani.

Kulingana na ripoti, mwanamke huyo ambaye ana mtoto mwingine naye anaishi Atlanta, Marekani ambako Davido amekuwa akitembea mara kwa mara katika ziara zake za Marekani.

Muda wa kuzaliwa kwa mtoto huyo ndio umewafanya wanamitandao kuonesha hasira. Inadaiwa ilitokea alipokuwa akifunga ndoa na Chioma wakati wote walikuwa na majonzi ya kifo cha mtoto wao.

Kuna madai zaidi kwamba Davido alijaribu kumpa mwanamke huyo shinikizo la kutoa mimba hiyo.

Kulingana na mdau wa ndani, Davido alisafiri kwa ndege hadi Amerika katika miezi ya mwanzoni mwa mwaka jana ili kutumia wakati mwingi na Amanda na binti yake wakati yeye na Chioma walikuwa wameachana.

Walakini, baada ya kifo cha Ifeanyi, familia ya Chioma ilisisitiza amuoe ili kuweza kumzika mwana wao.

Chanzo sasa kinadai Amanda tayari amejifungua mtoto, na Chioma amemuacha Davido kwa mara nyingine tena. Watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonyesha kukerwa baada ya kujua kuwa Davido amemfanyia Chioma yote hayo.

Msanii huyo amejibu katika ujumbe wa kimafumbo kwenye akaunti yake ya Twitter. Tetesi za kuenda nje ya ndoa zilimfanya aandike

"Juu ya watu wote."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved