Muigizaji mashuhuri wa Kenya Jacky Vike almaarufu Awinja Nyamwalo hayuko sokoni tena kufuatia harusi yake ya kitamaduni na mchekeshaji mwenzake Osoro.
Wawili hao walipeleka uhusiano wao katika hatua nyingine siku ya Jumamosi katika hafla ambayo ilipambwa na marafiki na wanafamilia wao wa karibu. Wakati wa hafla hiyo, Awinja na Osoro walikuwa wamevalia vitenge vilivyofanana.
Video zilizochukuliwa wakati wa hafla hiyo zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii, na kuibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki na wafuasi wao.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki walipuuza madai ya harusi hiyo, wengi wakisema kwamba huo ni mchezo mwingine wa ucheshi.
Kutokuwepo kwa marafiki mashuhuri wa Awinja kwenye sherehe hiyo ya kitamaduni kulizungumza mengi. Hii ilifanya iwe vigumu kwa mashabiki kuamini kwamba kweli Osoro na Awinja walikuwa wamefunga ndoa.
Kwa muda mrefu zaidi, Awinja na Osoro wamekuwa wakicheza mume na mke katika michezo yao mingi ya kuigiza - na kufanya iwe vigumu kwa mashabiki kuamini kuwa wao ni wapenzi.
Kufikia sasa video na picha zilizochukuliwa kwenye sherehe hiyo hazijachapishwa na watu wengine pekee - jambo ambalo limezua taharuki kwa mashabiki wanaohoji uhalali wa harusi hiyo ya kitamaduni.
Je, unaamini kwamba Awinja hayuko Sokoni? Muda pekee ndio utasema.
Hizi baadhi ya hisia za Wakenya:-
faithvoline Mko sure si jokes Za awinja za kila siku???
its.muthonii_ Mbona inakaa jokes๐๐๐
sta.muka Amber reeee, Akotheee, Kameneee, Sasa tena huyu... Soko mmesena mtaacha prity vishindo peke yake๐๐๐๐๐
jacintamumo19 Napenda venye ametupea suspense hapa๐๐๐hakuna mtu ako sure ni real ama ni comedy๐๐๐ tuwaache tu.๐
jacintamumo19 Napenda venye ametupea suspense hapa๐๐๐hakuna mtu ako sure ni real ama ni comedy๐๐๐ tuwaache tu.๐
iammariah9 Kumbe ilikua serious ivi ๐๐๐ and here I thought ilikua tu content ๐ฎ๐ฎ๐๐ aki shosho media wewe...love is a beautiful thing ๐๐๐ congrats to them
pascarlian Mko sure si comedy Bora nisione advertisement ya kitenge๐๐ anyway congratulations
mtunecessary Kutoka soko ndio ngumu kurudi requires only one text from that bitter ex and voila we are back to wearing boots while walking in the market
vanessa_maurine How are we supposed to believe this?๐๐๐๐
naomi.misoi Huyu Awinja anapenda jokes sana so hatujui kama hii iko serious or acting. Anyway congratulations if it's true
tessthebossbabe I though all along they were just creating content…nothing serious.Congratulations!๐ฅณ