"Hii ni nzuri!" Karen Nyamu ampongeza Akothee kwa kumsherehekea ex wake kwa ujumbe mtamu

“Akili ndogo kila mahali zinatafsiri maisha yetu. Akoth hii ni nzuril! Na heri ya siku ya kuzaliwa Nelly,” Karen Nyamu alimwambia Akothee.

Muhtasari

•Karen Nyamu amempongeza mwanamuziki  na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu Akothee baada ya kumsherehekea mpenzi wake wa zamani Nelly Oaks mnamo siku yake ya kuzaliwa.

•Mama huyo wa watoto watano alithamini ujumbe huo mzuri kutoka kwa seneta huyo na akaonyesha upendo kwake.

amempongeza Akothee kwa kumsherehekea Nelly Oaks
Karen Nyamu amempongeza Akothee kwa kumsherehekea Nelly Oaks
Image: HISANI

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu amempongeza mwanamuziki  na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu Akothee baada ya kumsherehekea mpenzi wake wa zamani Nelly Oaks mnamo siku yake ya kuzaliwa.

Bw Hezekiah Nelson Oyugi almaarufu Nelly Oaks ambaye mbali na kuwa mpenzi wa zamani wa Akothee pia ni meneja wake alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Ijumaa, Julai 7 na mama huyo wa watoto watano akamsherehekea kwa ujumbe mtamu.

Kama kawaida, Wakenya hawakuchelewa kutoa maoni kuhusu hatua ya mwanamuziki huyo kumsherehekea mpenzi wake wa zamani, baadhi wakimpongeza, wengine wakimkosoa na wengine hata wakiibua madai kwamba yeye na Nelly Oaks huenda bado wako na uhusiano wa kimapenzi. Wakili Karen Nyamu kwa upande wake alikuwa ujumbe wa pongezi kwa mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 na pia alichukua fursa hiyo kumtakia Nelly Oaks kheri njema ya siku ya kuzaliwa.

“Akili ndogo kila mahali zinatafsiri maisha yetu😂 Akoth hii ni nzuril! Na heri ya siku ya kuzaliwa Nelly,” Karen Nyamu alimwambia Akothee.

Mama huyo wa watoto watano alithamini ujumbe huo mzuri kutoka kwa seneta huyo na akaonyesha upendo kwake.

Katika taarifa ndefu kwenye mtandao wa Facebook siku ya Ijumaa, Akothee alimmwagia sifa kemkem meneja wake Nelly Oaks kwa jukumu kubwa ambalo amecheza katika maisha yake na biashara yake ya sanaa.

Alimshukuru mpenzi huyo wake wa zamani kwa kumsaidia kujenga jina lake na kumlinda alipokabiliwa na matatizo.

“Asante sana kwa sehemu uliyocheza katika maisha yangu yote na kazi yangu, ni sisi wawili tu tunaojua jinsi tulivyoipata brabd hapo ilipo. Asante sana kwa kuwepo wakati ulimwengu ulionekana kama damu ndani ya giza. Asante kwa kunifuta machozi, kusimama pamoja nami wakati baba wa watoto walipokusanyika dhidi yangu huko Uswizi, hiyo ilikuwa MBAYA. Unasimama nami,” Akothee alimwandikia Nelly Oaks kupitia ukurasa wake wa Facebook siku ya Ijumaa.

Aliongeza, "Unakumbuka bilione akiniambia niache muziki, nifute chaneli yangu ya YouTube, nifute akaunti zangu za mitandao ya kijamii na nibaki nyumbani?? Ulisimama kidete kumshawishi kuwa brand soon itajitengenezea pesa zake sio kupoteza muda wala kupoteza pesa, Tena asante kwa kuniamini. Ulinilinda mimi na brand kama tulikuwa mapacha.”

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alimhakikishia Nelly Oaks kwamba licha ya kilichotokea, bado yuko katika mioyo na akili za watoto wake.

“Ulianzisha uhusiano nao na bado unawatunza katika Nairobi yenye sumu, wewe ni familia. Kwa wale ambao hawajui, tunashiriki asili dhabiti ya familia na kwamba hakuna kinachoweza kutuvunja, "aliandika.

Akothee alithibisha kutengana na Nelly Oaks katikati mwa mwaka jana baada ya wawili hao kuwa kwenye mahusiano kwa muda.