Justina Syokau ni msanii Maarufu wa Kenya na wimbo maarufu kama 2020 na zingine. Anajulikana kwa nyimbo zake nyingi za kipekee na ustadi mzuri wa kucheza
Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook, ameshiriki kuwa hayuko sawa na amechoka kudanganya kuwa yuko sawa.
Katika chapisho refu, ameeleza jinsi mume wake wa zamani alivyokuwa jeuri na hamuungi mkono mtoto wao wa kiume, Nixon hata baada ya kumpeleka mahakamani mara kadhaa.
Katika chapisho hilo pia amefichua kuwa mumewe wa zamani ni kakake Kalonzo Musyoka.
Msanii huyo wa anasema kuwa babake mtoto alikoma kumsaidia mwanawe, licha yake kufukuza baada ya kujifungua.
"Nimechoka kudanganya siko sawa jina la x wangu ni Johnstone Vundi Musyoka Ndugu kwa kalonzo Musyoka Alinioa 2012 June akanifukuza 2013 Agosti Kwa pamoja tulipata mtoto wa kiume kwa jina NIXON MUSYOKA VUNDI Alinifukuza nje ya nyumba yetu ya ndoa Mara moja nilipojifungua mtoto wetu wa kiume
Mama yake anasema mwanae hatatunzwa na x wangu Mama kwa mume wangu jina lake ni MULLY Mwanamke huyu alinitendea vibaya alinitishia kumuacha mwanawe x wangu anafanya kazi wizara ya mambo ya nje Gereza eneo la industrial area yeye ni afisa wa bwana Alinifukuza aliendelea kutishia kuniua Hiyo ilinisukuma kwenda mahakamani
Aliitwa na mahakama Wakati huo alikubali kulipa 3500 kwa ajili ya mtoto wake Kisha mahakama ikaamuru alipe 8k kwa mwezi."
Syokau alieleza jinsi alivyorudi mahakamani mara kwa mara ili kumlazimisha aliyekuwa mume wake kumtunza mwanawe.
Amesema kwamba alichoka sana kumkumbusha kila mara kumtunza mwanawe.
Syokau alidai kwamba baba ya mtoto wake amekuwa akiwalipa watu kumnyanyasa mitandaoni,huku akisema kwamba amepitia mengi na mwanawe kwa ajili ya x wake.
Msanii huyo amekiri kwamba mwanawe hajui kama ana baba kwani hajawahi muuliza kuhusu baba yake.
"Mwanangu hajui kama ana baba,Wakati baba yake yuko hai sana ðŸ˜ðŸ˜ nimekejeliwa sana kwenye mitandao ya kijamii Wakati ninatafuta utunzaji kwa mtoto wangu Mwanangu hajawahi kuniuliza kuhusu baba yake kwa sababu hamjui baba yake Tulitengana kwa sababu alikuwa akinipiga
Alinidhalilisha sana Nilishuka moyo katika nyumba yangu mwenyewe sikuweza kutoka kwa sababu watu walitujua Sikuweza hata kuwaambia watu nini kilienda vibaya Nilinyamaza kimya,"Syokau alidai