Mwanaume mmoja aoa wake saba siku moja Uganda

Nsikonnene aefanya kijiji hiho kuenea kwa ramani ya sifa

Muhtasari

• Nsikonnene, aligonga vichwa vya habari baada ya kukutana na wazazi wa watarajiwa wake saba katika muda wa wiki moja.

 

Jamaa mmoja ambaye ni daktari wa mitishamba, mwenye umri wa miaka 43 kutoka kijiji cha Namasengere Wilaya ya Mukono nchini Uganda amekuwa akigonga vichwa vya habari baada ya kuoa wake saba kwa mpigo.

Habib Nsikonnene angeenda mbali zaidi kwa kuwa mmoja na wachumba wake saba, wawili kati yao wakiwa dada wa  toka nitoke, siku hiyo hiyo kufuatia harusi za kitamaduni za Kiislamu (Nikkah) zilizoandaliwa katika kila nyumba ya bibi arusi.

Nsikonnene, ambaye anasemekana kuwa na mifuko mirefu kulingana na viwango vya eneo hilo, basi angewakaribisha wake zake wote saba na marafiki zao na familia siku ya Jumapili kwenye hafla ya kukumbukwa ya mapokezi iliyofanyika nyumbani kwake kabla ya kuhamia pamoja na wake zake wote.

Inasemekana kuwa msafara wake wa ndoa ulikuwa na takriban magari 40 na pikipiki 30 kulingana na wakazi wa eneo hilo wanaosema kuwa biashara ya Nsikonnene inaingiza pesa nyingi.

Kwa wakazi wa eneo hilo, Nsikonnene amekuwa shujaa wa ibada baada ya kuweka kijiji chake kwenye ramani.

Image: HISANI

Emmanuel Owere, Mwenyekiti wa Kijiji cha Namasengere,aliezeza kuwa.

“Huyu mtu mwenye sifa adimu (Nsikonnene) aliishi katika kijiji hiki takriban miaka minne iliyopita, alikuja na kununua ardhi hapa na kujitambulisha kwangu kuwa yeye ni mganga wa kienyeji, tukamruhusu kufanya biashara yake,”

Aliongeza kusema kuwa;"Alipoishi hapa, hatukujua kwamba angetuletea umaarufu. Jina la kijiji chetu linavuma kila mahali."

Huku wananchi wakimpa sifa kedekede, Mwenyekiti wa kijiji  hicho sasa anataka kutaja barabara katika eneo hilo jina la Nsikonene. 

“Ni mtu adimu kwa sababu kutokana na hadhi yake katika jamii amekuwa akitangamana na kila mtu, ni mchapakazi na wenyeji wanapaswa kumwiga,” alisema Owere.