logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ex wa Harmonize, Kajala Masanja apewa onyo kali na mchumba wake baada ya kuchumbiwa

Kajala ameonywa na mchumba wake dhidi ya kuposti picha  zake za mazoezi kwenye mitandao ya kijamii.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani12 October 2023 - 04:54

Muhtasari


  • •Kajala hata hivyo alidokeza kuwa hayuko tayari kuacha tabia hiyo ambayo tayari ameshaizoea na anaonekana kuipenda.
  • •Kajala alionyesha akijiburudisha kwenye gym na kukejeli jinsi alivyoonywa dhidi ya tabia hiyo lakini hawezi kujizuia kufanya hivyo.

Aliyekuwa mpenzi wa mwimbaji Harmonize, Frida Kajala Masanja ameonywa na mchumba wake dhidi ya kuposti picha na video zake za mazoezi kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Siku ya Jumatano, muigizaji huyo mkongwe wa filamu bongo hata hivyo alidokeza kuwa hayuko tayari kuacha tabia hiyo ambayo tayari ameshaizoea na anaonekana kuipenda.

Kajala alichapisha video inayomuonyesha akijiburudisha kwenye ukumbi wa mazoezi na kukejeli jinsi alivyoonywa dhidi ya tabia hiyo lakini hawezi kujizuia kufanya hivyo.

“Pale baby anakwambia usipost ukienda gym, mimi sasa?!,” aliandika Kajala kwenye video hiyo.

Katika video hiyo, mama huyo wa binti mmoja alionekana akijiangalia kwenye kioo cha ukumbi wa mazoezi huku akirekodi kwa kutumia simu yake.

Haya yanajiri siku chache baada ya muigizaji huyo kuchumbiwa rasmi na mpenzi wake ambaye bado hajaweka wazi utambulisho wake.

Posti ya mapema wiki hii ya ex huyo wa Harmonize kwenye Instagram ilidokeza amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake.

Jumatatu, muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alichapisha video ya mkono wake wa kushoto ukiwa na pete kwenye kidole cha pete na katika sehemu ya maelezo akaeleza kuwa amechukuliwa na ameridhika.

"Mkono wangu unajisikia mzito leo... Nashangaa kwa nini.. Nimechukuliwa na kufurahi," Kajala aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuambatanisha ujumbe huo kwa emoji ya moyo kuashiria mapenzi.

Wiki ambayo ilipita, mama huyo wa binti mmoja alidokeza kwamba tayari anachumbiana na mwanamume mwingine na kwamba wako kwenye uhusiano wenye furaha.

Jumatano wiki jana, Kajala alishare ujumbe akidokeza kwamba amepata mwanamume ambaye anamtaka na kubainisha kwamba ameridhika. 

“Nimepata mwanaume ninayemtaka, nimefurahi,” ujumbe huo ulioshirikishwa na Kajala kwenye Instastori ulisomeka.

Muigizaji huyo hata hivyo hakushiriki maelezo zaidi kuhusu uhusiano wake mpya au mwanaume ambaye amechukua nafasi ya Harmonize. 

Haya yanajiri takriban miezi kumi baada ya uhusiano wake na bosi wa Konde Music Worldwide kufika kikomo baada ya kuchumbiana miezi kadhaa. Mastaa hao walikuwa wamerudiana mwezi Mei mwaka uliopita baada ya kutengana mwaka mmoja kabla. Harmonize alifanya juhudi nyingi kumuomba msamaha Kajala na kumtongoza katika juhudi za kumshawishi akubali kufufua uhusiano wao uliovunjika.

Wakati akitangaza kuachana na mwanamuziki huyo mwezi Desemba, Kajala aliweka wazi kwamba alikuwa tayari kupiga hatua nyingine baada ya mahusiano yao ya miezi michache kugonga mwamba.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved