logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tuliachana na mpenzi wangu sasa amenunua mbwa na kumpa jina langu - Jamaa alia

"Alinunua watoto wawili wa mbwa na kumpa yule wa kike jina la mpenzi wangu wa sasa na kumpa wa kiume jina langu.”

image
na Davis Ojiambo

Burudani25 October 2023 - 10:42

Muhtasari


  • • Mbaya Zaidi, mpenzi huyo wa zamani alinunua mbwa wawili, wa kike na wa kiume na kuwapa majina ya jamaa huyo na mwngine jina la mpenzi wa sasa wa jamaa huyo.
Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi

Mwanamume mmoja katika mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter ameelezea kuchukizwa kwake na kitendo alichomfanyia mpenzi wake wa zamani.

Kwa mujibu wa mwanamume huyo, alieleza kwamba mpenzi wake wa zamani baada ya kuachana, alinunua mbwa na kumpa jina la jamaa huyo, akisema kwamba hatua hiyo imemkwaza sana.

Mwanamume huyo alisema kinachomuuma Zaidi ni kwamba mpenzi huyo wake anaishi mbali wa mita chache kutoka kwa nyumba yake na kila mara anapopita anamuona na kuanza kuita mbwa wake kwa jina lake.

Mbaya Zaidi, mpenzi huyo wa zamani alinunua mbwa wawili, wa kike na wa kiume na kuwapa majina ya jamaa huyo na mwngine jina la mpenzi wa sasa wa jamaa huyo.

“Mpenzi wangu wa zamani anaishi mtaa mbali kidogo kutoka nyumbani kwangu, tuliachana miezi michache iliyopita, mara baada ya kugundua kuwa nilikuwa natoka na mtu mwingine, alinunua watoto wawili wa mbwa na kumpa yule wa kike jina la mpenzi wangu wa sasa na kumpa wa kiume jina langu.”

“Shida ni kwamba watoto wa mbwa wamekua kabisa, na wanazaliana. Kila puppy jike anapozaa, huwapa watoto hao majina ya familia yangu yote. Sisi ni kicheko katika jamii." Alieleza kwenye ujumbe huo uliosambazwa na mtumizi mmoja wa Twitter kwa jina Postsubmann.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved