Vijana Single wafanya crusade kuomba Mungu awape wapenzi kabla mwaka kuisha (video)

Katika video hiyo, vijana wengi wanaoaminika kuwa hawajaoa walionekana kwenye mkusanyiko mkubwa, wakichanganyika na eti wakisali.

Muhtasari

• Baadhi ya vijana walikuwa kwenye makundi, wakipiga soga na pengine kufahamiana, kwani nukuu ya video hiyo ilipendekeza pia ilikuwa fursa ya kukutana na kusalimiana.

Mkutano wa singles
Mkutano wa singles
Image: TikTok

Mamia ya vijana ambao hawana wapenzi na wamefikia umri wa kuoa au kuolewa wamefurika kaitka kongamano la ibada ya maombi kutuma vilio vyao kwa Mungu kuwajaalia wapenzi kabla ya kumalizika kwa mwaka 2023, ikiwa imesalia miezi miwili tu.

Mkutano wa maombi ulinaswa katika video iliyowekwa kwenye TikTok na mtumizi mmoja wa mtandao huo wa klipu fupi kwa jina Mama Zion, ambaye alisema pia ilikuwa fursa ya kukutana na kusalimiana.

Katika video hiyo, vijana wengi wanaoaminika kuwa hawajaoa walionekana kwenye mkusanyiko mkubwa, wakichanganyika na eti wakisali. Baadhi ya vijana walikuwa kwenye makundi, wakipiga soga na pengine kufahamiana, kwani nukuu ya video hiyo ilipendekeza pia ilikuwa fursa ya kukutana na kusalimiana kama njia moja ya pengine kupata mwenza wako.

Video hiyo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuvutia maoni tofauti kutoka kwa watumiaji wa mtandao. Wakati baadhi ya watu walikuwa na maoni kwamba kuombea mwenzi wa maisha sio kosa, wengine walisema walishuku kungekuwa na wanawake wengi kwenye mkutano huo.

Mkutano huo hata hivyo pia haukujulikana ulifanyika katika taifa lipi a Afrika lakini unakuja wakati ambapo utafiti unaonesha kwamba vijana wengi walio katika mabano ya kuoa au kuolewa hawataki tena kufanya jambo hilo la heri.

Kwa mujibu wa tafiti mbali mbali, vijana wengi wamekuwa na woga wa kuingia katika ndoa kwa kuona jinsi ambavyo kumekuwa na talaka nyingi na visa vingi pia vya dhuluma za kinyumbani na kijinsia.