Simulizi moja ambayo imewaacha wengi kuzungumza katika mtandao wa X inawahusisha wapenzi kutoka nchini Nigeria ambao mwanamume alitaka kumhonga mpenziwe waliyekaa naye kwa miaka 7 ili kuvunja penzi lao.
Kwa mujibu wa msumulizi, alisema kuwa alisimulia tukio hilo na mrembo huyo baada ya mwanamume wake kumfuata akitaka waachane, lakini si mikono mitupu.
Jamaa huyo alikuwa radhi kumlipa mrembo wake kiasi cha Naira milioni 5 ambazo ni sawa na laki 8 na nusu pesa za Kenya ili wawezec kuvunja penzi lao.
Mwanamume huyo alimuelezea mrembo wa watu kwamba asingeendelea kukaa na yeye tena kimapenzi kwani ameshampata mzuri wa kumtambulisha kwa wazazi wake, hivyo akamtaka kukubali laki 8 kama fidia ya kumharibia muda wake – miaka 7.
Hata hivyo, msimulizi aliwashangaza wengi baada ya mrembo huyo kumwambia kwamba alikuwa anatathmini kukataa kuchukua kiasi hicho cha pesa, akisema kuwa hakuna kiasi chochote cha pesa kitakachoweza kununua muda wote ambao amemharibia.
“Rafiki amekuwa akichumbiana na mvulana huyu kwa miaka 7 na sasa amepata mtu mwingine na anampa N5 milioni ili asiendelee kuwa mpenzi wake. Anafikiria kuondoka bila kukusanya hata senti kutoka kwake,” msimulizi alisema.
Baadhi ya watumizi katika jukwaa hilo la mijadala walimshauri mrembo huyo kuchukua pesa na mengine kufuata baadae, huku wengine wakimhurumia kwa kuharibiwa muda wa takribani mwongo mmoja.
“Mamaa kusanya pesa ufurahie, mengine watafuata. Acha ujinga, hakuna anayekataa pesa iliyotolewa bure,” mmoja alimwaambia.
“Wanaume siku zote wanatuvunja moyo wakati ambao hutarajii, ila dada usiache hela,” mwingine alimwambia.