logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Njaanuari: Jamaa afutwa kazi kwa kukataa ku'share chakula chake na meneja wake kazini

Bosi huyo alikuwa na mazoea ya kuzunguka kila mezi akidokoa chakula cha kila mfanyakazi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani10 January 2024 - 10:00

Muhtasari


  • • Bosi huyo alikuwa na mazoea ya kuzunguka kila mezi akidokoa chakula cha kila mfanyakazi.
Jamaa asimulia kufutwa kwa kukataa bosi asionje chakula chake kazini

Mwanaume mmoja katika jukwaa la X, aliyetambulika kwa jina la Somto Ihezue amewashangaza watumizi wa mtandao huo baada ya kufichua sababu ambayo ilipelekea yeye kupoteza kazi.

Jamaa huyo alisema alipoteza kazi muda mfupi baada ya kukataa jaribio la bosi wake kuonja chakula chake cha mchana.

Mwanamume huyo, ambaye sasa ameajiriwa mahali pengine, alisimulia uzoefu wa zamani kutoka kwa kazi yake ya awali na kueleza kwa kina kile anachofikiri kilisababisha kufutwa kwake na bosi wake wa zamani.

Somto alisimulia kuwa tukio hilo lilitokea siku maalum ambapo bosi wake ambaye alikuwa anapenda kula chakula cha wafanyakazi, alianza kuonja chakula cha kila mtu mmoja baada ya mwingine.

Lakini kabla haijafika zamu yake, alikinyanyua chakula chake haraka ili asionje bosi wake.

Hata hivyo, bosi wake alijua hili na akamtazama machoni kwa sura ya kusikitisha, na wiki moja tu baada ya hapo, alifukuzwa na bosi huyo kwa kutokuwa na ushirikiano mwema na wenzake kazini.

Aliandika, “Nilifukuzwa kazini kwa sababu sikumruhusu meneja kula chakula changu cha mchana. Siku zote alizunguka kula chakula cha mchana cha kila mtu, kwa hiyo siku moja, nilikusanya haraka chakula changu kabla hajanifikia. Alinitazama kwa muda mrefu, kwa hasira. Nilifukuzwa kazi wiki iliyofuata.”

Chapisho hilo lilivutia maoni mbali mbali ya kuchekesha huku wengine wakimpongeza kwa kupata kazi kwingine na kukwepa mazoea ya bosi huyo kupe.

“Natumai ulichukua jina lake kwa dibia au mungu au mtu yeyote tbh kwa sababu huyo alikuwa akitangaza vita,” Chikamma alimwambia.

“Huu ni wazimu, lakini tena inaweza kuwa njia moja ambayo Mungu alitumia kukuepusha na kupe wa meneja, huh,” mmoja alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved