Mtayarishi wa maudhui mashuhuri wa Kenya Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy ameweka wazi kuwa hana mpango wa kupata watoto kwa sasa.
Wakati akiwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22 alidokeza kuwa atajifungua tu wakati atakapokuwa tayari, na atakapokuwa amepanga kupata watoto.
Katika kipindi hicho cha siku ya Jumamosi, shabiki alitaka kujua ni lini mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji Stevo Simple Boy anapanga kuolewa na kuwa na familia.
“Unaolewa lini na kupata angalau mtoto?" Shabiki aliuliza.
Katika majibu yake, Pritty Vishy alitoa mfano wa mama yake mzazi ambaye alifichua alijifungua watoto wanne ambao hakuwa amepangia, na kubainishwa kwamba hataki kufuata njia hiyo.
‘Weeeh, si mnataka niolewe na nizae. Sitapata mtoto kama siko tayari,” Pritty Vishy alijibu.
Aliongeza, “Zaidi ya hayo nataka mtoto aliyepangiwa. Sitaki kuwa kama mama yangu ambaye alikuwa na watoto wanne na wote hawajapangiwa. "Hakuna cha kibinafsi, asante."
Wakati akimjibu shabiki mwingine aliyeuliza swali kama hilo la kupata watoto, hata hivyo alidokeza kuwa kuna mtu ambaye anaweza kufikiria kuzaa naye.
"Mpango wangu ulikuwa labda kamwe (kutopata watoto) lakini kuna mtu huyu.," alisema.
Vishy alipoulizwa kama yuko kwenye uhusiano wowote, alionekana kukwepa swali hilo na kujibu, "Na leo rada ni mangais gani?"
Mtayarishaji wa maudhui huyo mwenye umri wa miaka 22 pia alizungumza kuhusu mipango yake ya siku ya Wapendanao akisema, "Nataka kuzurura kaa ng'ombe za wamasai."
Katikati mwa mwaka jana, mpenzi huyo wa zamani wa Stevo Simple Boy alikuwa amedokeza kwamba amezama kabisa ndani ya dimbwi la mahaba na mcheza santuri wa Kenya ambaye anaishi Marekani.
Mwezi Mei, alichapisha picha za mcheza santuri huyo anayefahamika kwa jina DJ Starvy na kunukuu kwa maneno matamu kwake
"Ninapenda kila kitu kuhusu wewe. Unafanya kila kitu kizuri. Unajua unanifanya kichaa, sawa? Nakupenda babe @dj_starvy," alisema.
Starvy alijibu kwa kumhakikishia kipusa huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhusu mapenzi yake makubwa kwake.
"Unajua nakupenda mama watoto," alisema.
Vishy aliendelea, "Nakupea watoto 8 mapacha ndani na kadhalika."