logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kelvin Kinuthia afunguka kuhusu utambulisho wake, afichua kwa nini hapendi kuitwa 'bro'

Kinuthia alisema huwa inahisi mbaya watu wanapomwita 'bro' na kuwataka wamtambue tu 'Kinuthia' au 'baby girl'.

image
na Samuel Maina

Burudani07 April 2024 - 06:47

Muhtasari


  • •Mtumbuizaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alisisitiza kuwa hapendi kuitwa 'bro', jina maarufu ambalo Wakenya huwaita marafiki zao wa kiume.
  • •Kinuthia alisema huwa inahisi mbaya watu wanapomwita 'bro' na kuwataka wamtambue tu 'Kinuthia' au 'baby girl'.

Mtayarishaji wa maudhui maarufu wa Kenya anayejulikana zaidi kwa kuvaa nguo za wanaume na wanawake, Kelvin Kinuthia amefunguka kuhusu jinsi ambavyo angependa kutambuliwa.

Katika mahojiano na Mungai Eve, mtumbuizaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alisisitiza kuwa hapendi kuitwa 'bro', jina maarufu ambalo Wakenya huwaita marafiki zao wa kiume.

Mtayarishaji huyo wa maudhui hayo alisema huwa inahisi mbaya watu wanapomwita 'bro' na kuwataka wamtambue tu 'Kinuthia' au 'baby girl'.

“Siwezi kusema huwa nakasirika, inaonekana ni mbaya, fikiria umeng’ara upo katikati ya mall mtu anakuita kwa sauti ‘niaje bro’ anahisi haifai, Ata watu wanaweza baki wakiangalia ni nani huyo anaitwa bro. Watu wanamtafuta wanamkosa," Kinuthia alisema.

Aliongeza, "Mimi huwa nasema, nadhani ni mbaya, naona haifai. Niite tu Kinuthia, ukiona 'baby girl' ni mbaya, niite 'Kinuthia sasa'."

Kinuthia alibainisha kuwa tayari watu wameanza kukumbatiana kumwita ‘baby girl’ tangu alipolalamika kwa mara ya kwanza dhidi ya kuitwa ‘bro’.

“Nadhani imepungua coz siku hii nakutana na watu wananiita baby girl, naona meseji moja ilipokelewa vizuri,” alisema.

Pia alibainisha kuwa yeye hajali kurejelewa kwa viwakilishi vya kiume au vya kike, akibainisha kuwa hakuna ambavyo vinaweza kumuudhi.

"Sina shida kutambulika kwa kutumia kiwakilishi chochote. Watu hushindwa wataniita aje. Au baada ya kuniita ‘bro’, niite tu "wee", alisema.

“Kila kiwakilishi kipo sawa, ukitaka kutumia ‘he’ tumia, ukitaka kutumia ‘she’ ni sawa, sitakerwa na hilo,” aliongeza.

Katika siku za nyuma, mtayarishaji huyo wa maudhui ya TikTok na YouTube aliwahi kuweka wazi kuwa yeye ni mwanaume.

Akiwa kwenye mahojiano, Kinuthia alisema kucheza uhusika wa kike kwenye video zake ni kwa ajili ya burudani na kazi tu.

Kinuthia alibainisha kuwa kamwe hajawahi kukana jinsia yake ya kiume. Hata hivyo aliweka wazi kuwa hayupo tayari kuacha kuigiza kama mwanamke kwa kuwa hiyo ndiyo riziki yake.

"Mimi ni mwanaume. Lakini nilisema siwezi wacha kufanya vitu nafanya kwa sababu watu wameniingililia ati nafanya vile na mimi ni mwanaume. Hiyo ndiyo imenifikisha mahali nipo," Kinuthia alisema katika mahojiano na Eve Mungai.

Mwanatiktok huyo alisema amekuwa akikejeliwa sana mitandaoni kwa kuigiza kama mwanamke ilhali yeye ni mwanaume.

Hata hivyo alidai kuwa nafasi hiyo ya kike ambayo anacheza imefanya apate kazi za kufanya matangazo ya mavazi na mapambo ya kike.

"Hakuna vile nitaanza kubadilisha mhusika. Hata watu wataboeka. Kuna watu tayari wamezoea jinsi Kinuthia alivyo. Hakuna mahali ambapo nimewahi kusema kuwa mimi sio mwanaume. Ni kazi na hiyo ndiyo imenifikisha mahali nilipo," Alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved