Mwanamke mmoja amezua hisia kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba kwake kumuamini mwanamume ni vigumu.
Mrembo huyo alisema kwamba endapo atatakiwa kufanya chaguo kati ya kuamini mwanamume au kuanza kuhesabu nafaka za mchele moja baada ya nyingine, basi yuko radhi kuhesabu nafaka za mcheke hata kama ni gumia mzima.
Katika chapisho lililoshirikiwa kwenye ukurasa wake, alionyesha uso wake kando ya trei ya nafaka za mchele zilizopangwa kwa uangalifu.
Maneno hayo yalisomeka: ‘Waamini wanaume au panga mchele.’ Muda mfupi baadaye, alionekana kwenye video akihesabu na kupanga nafaka kwenye trei.
Video hiyo ilipata umakini haraka kwenye mitandao ya kijamii na kuvutia hisia kinzani, baadhi wakihoji ni vipi vidosho wamepoteza Imani zao kwa wanaume kwa haraka.
Hii hapa video;