Mwanamume mwenye hasira amefichua kwamba alimuadhibu mkewe kisiri baada ya kugundua anachepuka na wanaume wengine.
Mume huyo alisimulia kwamba aligundua mkewe alichepuka na wanaume wawili kwenye mapenzi siku iliyopita na akaamua kumfanyia kitendo ambacho hatosahau.
Ili kukabiliana naye, aliidukua simu yake na kuiba kila senti iliyokuwa kwenye akaunti zake za pesa bila mke kujua nini kinaendelea.
Hakuishia hapo, kisha alichukua vyeti vya mkewe vyote na kuviteketeza moto na baadae kujifanya hajui vilipotelea wapi.
Hadithi yake ilitumwa kwa X influencer @Wizarab10 kama ujumbe usiojulikana na iliwakasirisha watu.
Mume huyo alitetea hatua hiyo akisema kwamba yeye ni mmoja wa watu wanaoamini katika falsafa ya kwamba hakuna kosa linalostahili kupita tu bila kuadhibiwa.
“Nimegundua kwamba mke wangu alifanya threesome jana, hivi sasa hajui kama niligundua. Mimi pia kwa upande wangu naamini kwamba katika kila tukio, lazima kuna madhara. Simu yake imedukuliwa na salio lote kukombwa bila yeye kujua. Vyeti vyake pia vimetoweka, vimechomwa,” alisema mume huyo.
Hili lilivutia maoni kinzani baadhi wakimtuhumu kwa kufanya hivyo kama njia ya kulipa kisasi huku wengine wakimpongeza kwa kumpa funzo ambalo hatokuja kulisahau.
“Natumaini hukufanya mambo hayo yote ili kumrudia. Songa mbele na umuache kwenye maisha yake ya kudanganya kama mwanamume mkomavu,” mmoja alisema.
“Umechoma cheti cha shule kwa sababu alikulaghai?? Una wazimu o” mwingine alisema.
“This is evilness please this better be a joke though, kwanini uchome cheti chake cuz she had threesome!?”
“Hata nafsi haitoshi. Unaweza kumtia sumu kinywaji au chakula chake” mwingine alimshauri vibaya.