"Tunarudi kama mume na mke!" Akothee atangaza baada ya safari ya Uganda na Nelly Oaks

Asante sana Uganda, umeimarisha maisha yangu ya Upendo. Nakupenda Uganda,” Akothee alisema.

Muhtasari

•Msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 alifichua kwamba yeye na Nelly Oaks walifanya upya viapo vyao, kuwafanya mume na mke.

•Aliendelea kutangaza kwamba atasafiri kurudi huko hivi karibuni.

Akothee na aliyekuwa mpenzi wake Nelly Oaks
Akothee na aliyekuwa mpenzi wake Nelly Oaks
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu Akothee amezungumza kuhusu mafanikio ya safari yake ya hivi majuzi nchini Uganda na meneja wake Nelly Oaks.

Katika chapisho la Jumatatu jioni, msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 alifichua kwamba yeye na Nelly Oaks walifanya upya viapo vyao, kuwafanya mume na mke.

Alitoa shukrani zake kwa nchi hiyo jirani akikiri kwamba mapenzi yao yaliimarishwa huko.

“Yooo Uganda walituharibu, tulienda kama meneja na msanii, tunarudi nyumbani kama mke na mume. Je, Uliona viapo vyetu vikifanywa upya Uganda? Asante sana Uganda, umeimarisha maisha yangu ya Upendo. Nakupenda Uganda,” Akothee aliandika.

Aliendelea kutangaza kwamba atasafiri kurudi huko hivi karibuni.

Katika siku chache zilizopita, Akothee na mpenzi wake Nelly Oaks, ambaye pia ni meneja wake rasmi, wamekuwa katika safari inayohusiana na utalii nchini Uganda. Wawili hao wamekuwa wakisherehekea mapenzi yao waziwazi katika miezi kadhaa iliyopita, baada ya kurudiana tena kufuatia kuvunjika kwa ndoa ya Akothee na Denis Schweizer katikati mwa mwaka uliopita.

Mwishoni mwa mwaka jana, mwanamuziki huyo alionekana kuthibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na mNelly Oaks katika kipindi cha moja kwa moja cha hivi majuzi kwenye mtandao wa TikTok.

Katika kipindi hicho ambacho alikuwa akiwahutubia mashabiki wake Nelly Oaks akimwandalia chakula maalum jikoni, Akothee alisikika akimwita meneja huyo wake ‘babe’ mara kadhaa, jina ambalo hutumika sana sana  wapenzi.

Nelly Oaks pia alisikika akimtaja Akothee kama mtu maalum kwake huku wawili hao wakishiriki matukio ya kimapenzi kwenye kamera.

“Hiki ni chakula cha jioni maalum kwa mtu maalum kama wewe. Ni surprise,” Nelly Oaks alisikika akimwambia mwanamuziki huyo.

Wakati wa kipindi hicho, Akothee kwa hasira aliwasuta wanawake wote waliokiri mapenzi yao kwa meneja huyo wake akidokeza kuwa hapatikani kwao.

Wakati baadhi ya mashabiki walipotaka kujua iwapo Nelly Oaks ana mchumba, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alionekana kuthibitisha kuwa yeye ndiye anashikilia nafasi hiyo.

“Ati kama Nelly ako na mtu?! Kwani mimi mawe? Mimi mawe? Ama mimi ni mti? Unauliza kama Nelly ako na mtu, kwani mimi ni mawe? Ama kijiti? Usinipimie pumzi. Maisha ni ya kwangu nayaendesha vile nataka,” alisema.

Mama huyo wa watoto watano pia alikataa ombi la nambari ya simu ya Nelly Oaks huku akifichua kwamba hata ana uwezo wa kufungua na kutumia simu yake.

“Kweli nikupatie namba ya Nelly? unadhani mimi nimetosheka? Mimi sijarudi soko, mimi ndiye soko, sigawani na mtu,” Akothee alisema.

Nelly Oaks pia aliweka wazi kuwa hapatikani kwa mwanamke mwingine