Mchungaji
na mwimbaji wa nyimbo za injili Linet Munyali almaarufu Size 8 Reborn
ameonekana kukiri kwamba alikuwa amezama sana katika raha za kidunia kabla ya
kuchukua hatua ya kukokoka miaka mingi iliyopita.
Mama
huyo wa watoto wawili alitoa maisha yake kwa Yesu Kristo zaidi ya mwongo mmoja
uliopita, katika kipindi ambacho alifunga ndoa na mcheza santuri Samuel Muraya
almaarufu DJ Mo.
Katika
chapisho la hivi majuzi, alionyesha picha zake za kumbukumbu zinazoonyesha
alipokuwa angali katika tasnia ya muziki wa kilimwengu na katika sehemu ya
maelezo, alisherehekea Mungu kumuondoa mahali hapo.
“Alikonitoa
katikati ya madawa, usherati na pombe hiyo ilikua rada,” Size 8 alisema kwenye
picha ambazo alichapisha.
Aliongeza,
“Utukufu kwa Mungu, kwa rehema na neema zake alituokoa, nimeokoka.”
Size
8, ambaye alianza kama mwanamuziki wa kilimwengu akiachia vibao
vilivyomtambulisha kama mmoja wa wasanii mashuhuri wa kike, aliokoka mwaka wa
2012.
Ni
mwaka huo huo ambapo alifunga ndoa na DJ Mo ambaye wamezaa naye watoto wawili
pamoja.
Baada ya kuokoka, alijipatia jina jipya la Size 8 Reborn na kujitolea sana, ikiwa ni pamoja na kupeana baadhi ya vitu vyake vya thamani alivyokuwa amechuma kutoka kwa ulimwengu wa kilimwengu.
Chapisho
la hivi majuzi la mwimbaji huyo linakuja wakati ndoa yake inasemekana kuwa
imefikia kikomo.
Mwezi
uliopita, Size 8 alifunguka kuhusu uamuzi mzito wa kuvunja ndoa yake na DJ Mo,
wiki kadhaa baada ya kufichua kuwa hakuwa na mchumba.
Katika taarifa ya hisia kali, mwimbaji huyo alikiri kwamba licha ya maoni makali ya umma na uvumi mwingi, hisia zake kwa DJ Mo bado ni kubwa.
Hapo
awali, alikuwa amewashtua wafuasi wake kwa kutangaza kwamba sasa yupo single,
na hivyo kuashiria mwisho wa ndoa yao ya miaka 11.
Tangazo hilo lilikumbwa na mchanganyiko wa mshangao na mashaka, huku wengi wakihoji iwapo kutengana kwao ni kweli au ni taswira ya kiki.