logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu maelezo muhimu kuhusu mwanasoka Victor Wanyama na mpenzi wake Serah Teshna

Mahusiano ya mastaa hao wawili wa Kenya yamebaki kuwa faragha kwa miaka mingi.

image
na Samuel Mainajournalist

Dakia-udaku24 October 2024 - 12:09

Muhtasari


  • Nahodha wa zamani wa Harambee Stars Victor Mugubi Wanyama na mpenzi wake Serah Teshna wametangaza habari za kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili pamoja.
  • Ni machache mno ambayo wameweka hadharani.

Jumatano, nahodha wa zamani wa Harambee Stars Victor Mugubi Wanyama na mpenzi wake Serah Teshna walitangaza habari za kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili pamoja.

Katika chapisho kwenye akaunti zao za Instagram, wapenzi hao wawili wanaoishi Canada walifichua kuwa mtoto wao wa pili kwa jina Gigi alizaliwa takriban miezi mitano iliyopita.

Serah alionyesha picha ya Wanyama akiwa amelala chali kitandani huku mtoto huyo mchanga akitambaa kwenye mgongo wake na chini ya picha hiyo akasema;

“Gigi mdogo na baba. Miezi mitano iliyopita imejawa na upendo mwingi, furaha, joto, kicheko, machafuko kidogo ya hapa na pale na bila shaka usiku wa kukosa usingizi. Lakini tunaipenda hapa,” Serah alisema kwenye chapisho lake Jumatano jioni.

Muigizaji huyo mrembo aliendelea kueleza kuwa mtoto wao wa pili kwa pamoja amekamilisha familia yao na akamtambua kama zawadi kamilifu ya Mungu. Pia alieleza kuhusu furaha kubwa mioyoni mwao kuona mvulana huyo mchanga akicheza na mwana wao mkubwa na akasisitiza kwamba wanampenda sana.

"Almasi yetu ndogo imekamilisha mraba wetu mzuri. Kukutazama wewe na kaka mkubwa mkihusiana vyema ndio kila kitu tulichoomba. Hawezi kusubiri wewe kutembea na kucheza pamoja. Tunakupenda Gigi. Zawadi kamili ya Mungu. Miezi 5," alisema.

Ufichuzi huo unakuja wiki chache tu baada ya wanandoa hao kufichua kuhusu ujauzito wa pili wa Serah.

Mnamo Oktoba 10, Wanyama na Teshna walitangaza kwamba familia yao inaendelea kupanuka.

Mahusiano ya mastaa  hao wawili wa Kenya yamebaki kuwa faragha kwa miaka mingi. Ni machache mno ambayo wameweka hadharani.

Chini hapa tazama maelezo muhimu kuhusu Wanyama na mpenziwe Serah Teshna

• Wanyama ni mwanasoka anayechezea Montreal Impact.

• Serah ni muigizaji, na mtangazaji wa runinga.

• Wamekuwa pamoja kwa takriban miaka 8.

• Wameweka maelezo ya uhusiano wao faragha.

• Kwa sasa wanaishi Montreal, Kanada.

• Waliweka wazi uhusiano wao mwaka wa 2021.

• Walipata mtoto wa kwanza Septemba 2021.

• Walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wa pili Oktoba 23, miezi 5 baada ya kuzaliwa.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved