logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hongera! Victor Wanyama na mpenziwe Serah Teshna watangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili pamoja

"Miezi mitano iliyopita imejawa na upendo mwingi, furaha, joto, kicheko, machafuko kidogo ya hapa na pale na bila shaka usiku wa kukosa usingizi," Serah alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Dakia-udaku24 October 2024 - 07:24

Muhtasari


  • Katika chapisho kwenye Instagram, wapenzi hao wawili wanaoishi Canada walifichua kuwa mtoto wao wa pili kwa jina Gigi alizaliwa takriban miezi mitano iliyopita.
  • Serah alieleza kuwa mtoto wao wa pili kwa pamoja amekamilisha familia yao na akamtambua kama zawadi kamilifu ya Mungu.

Siku ya Jumatano, nahodha wa zamani wa Harambee Stars Victor Mugubi Wanyama na mpenzi wake Serah Teshna walitangaza habari za kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili pamoja.

Katika chapisho kwenye akaunti zao za Instagram, wapenzi hao wawili wanaoishi Canada walifichua kuwa mtoto wao wa pili kwa jina Gigi alizaliwa takriban miezi mitano iliyopita.

Serah alionyesha picha ya Wanyama akiwa amelala chali kitandani huku mtoto huyo mchanga akitambaa kwenye mgongo wake na chini ya picha hiyo akasema;

“Gigi mdogo na baba. Miezi mitano iliyopita imejawa na upendo mwingi, furaha, joto, kicheko, machafuko kidogo ya hapa na pale na bila shaka usiku wa kukosa usingizi. Lakini tunaipenda hapa,” Serah alisema kwenye chapisho lake Jumatano jioni.

Muigizaji huyo mrembo aliendelea kueleza kuwa mtoto wao wa pili kwa pamoja amekamilisha familia yao na akamtambua kama zawadi kamilifu ya Mungu.

Pia alieleza kuhusu furaha kubwa mioyoni mwao kuona mvulana huyo mchanga akicheza na mwana wao mkubwa na akasisitiza kwamba wanampenda sana.

"Almasi yetu ndogo imekamilisha mraba wetu mzuri. Kukutazama wewe na kaka mkubwa mkihusiana vyema ndio kila kitu tulichoomba. Hawezi kusubiri wewe kutembea na kucheza pamoja. Tunakupenda Gigi 🥰. Zawadi kamili ya Mungu 🎁 Miezi 5," alisema.

Ufichuzi huo unakuja wiki chache tu baada ya wanandoa hao kufichua kuhusu ujauzito wa pili wa Serah.

Mnamo Oktoba 10, Wanyama na Teshna walitangaza kwamba familia yao inaendelea kupanuka.

Serah mwenye furaha alitangaza kwamba alikuwa anatarajia mtoto wa pili katika familia yake. “Hapa Tunakua …… TENA!!!! “Oh, Mpenzi! Tunapata mtoto!!! Alifanya jambo hilo litendeke kwa wakati WAKE kamili. ATAFANYA HIVYO?? 🙏🏽🙏🏽♥️♥️♥️♥️,” Serah Teshna alisema.

Tangazo hilo la ujauzito lilivutia hisia nyingi kutoka kwa mashabiki wake na watu mashuhuri ambao waliwapongeza wanandoa hao.

Mastaa hao wawili wa Kenya wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 7 sasa na wana mtoto mwingine wa kiume pamoja ambaye ana miaka mitatu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved